Jifunze historia ya TANU kutoka maktaba ya Mohamed Shebe

Jifunze historia ya TANU kutoka maktaba ya Mohamed Shebe

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
JIFUNZE HISTORIA YA TANU KUTOKA MAKTABA YA MOHAMED SHEBE

Angalia umma uliokuwa unahudhuria mikutano ya TANU Mnazi Mmoja.

Nimefahamishwa kuwa shajara (diary) za Abdul Sykes zina hotuba za Nyerere (verbatim) katika short hand (hati mkato).

Bahati mbaya sana hizi shajara hadi leo hazijafunguliwa.

Niliziomba kuzisoma wakati wa utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes lakini sikupewa na niliziona kwa macho yangu nyumbani kwa mwanae marehemu Kleist.

Katika picha hiyo kuna sehemu kushoto inaonekana rangi nyeusi tupu.

Hao ni wanawake wa Kiislam waliokuwa wanahudhuria mikutano ya TANU walitengewa sehemu yao maalum.

Ilikuwa kazi kubwa sana kuwatoa akina mama uani kuwaleta Mnazi Mmoja uwanjani kuja kupiga vigelegele na kuzigeuza nyimbo za lelemama kuwa nyimbo za kuhamasisha wananchi dhidi ya ukoloni.

Mama Sakina (Bi. Chiku bint Said Kisusa) mke wa Shariff Abdallah Attas alifanya kazi kubwa akishirikiana na Bi. Titi Mohamed, Bi. Tatu bint Mzee na Bi. Hawa Maftah kuwaingiza wanawake katika TANU.

Picha ya pili niliowatambua nimewaandika majina yao kwenye picha - Sheikh Suleiman Takadir, Iddi Faiz Mafungo, John Rupia, Rashid Kawawa, Said Maswanya na Robert Makange.

Picha ya tatu Julius Nyerere anasalimiana na wananchi 1956.

Picha ya nne kulia Bi. Titi Mohamed, Mama Maria Nyerere, Julius Nyerere, Rashid Kawawa na nyuma ya Nyerere ni Tewa Said Tewa.

Picha TANU ni siku ya uhuru wa Tanganyika 9 Desemba 1961.

Julius Nyerere na Prince Philip kulia kabisa anaonekana Sheikh Abdalla Iddi Chaurembo.

1629132084853.png


1629132114266.png


1629132248923.png


1629132161293.png


1629132204902.png
 
Hiyo picha ipo wapi, alafu unaposema historia unatakiwa uwanzie msingi sasa hapa umekuja kutueeza tanu ishaundwa tunataka kujua nani alipata wazo la kuunda tanu, ilikuwaje ikaundwa walikuwa akina nani na nani, embu funguka muhenga
 
Hiyo picha ipo wapi, alafu unaposema historia unatakiwa uwanzie msingi sasa hapa umekuja kutueeza tanu ishaundwa tunataka kujua nani alipata wazo la kuunda tanu, ilikuwaje ikaundwa walikuwa akina nani na nani, embu funguka muhenga
Mbenda,
Inaelekea wewe ndugu yetu ni mgeni hapa barzani.

Makala ina picha tano kwangu zote zinaonekana.

Nimeweka tena picha ya mkutano wa TANU.

Tumejadili sana kuhusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Mimi unayenisoma hapa nimeandika kitabu, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," Minerva Press London 1998.

Fikra ya kuwaunganisha Waafrika ilitoka kwa Dr. Kweggiyr Aggrey kutoka Achimota College Ghana kumweleza Kleist Sykes alipokuja Tanganyika mwaka wa 1924.

1929 Kleist na marafiki zake akiwemo Cecil Matola, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamis, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Ali Mpima, Raikes Kusi na Rawson Watts wakaunda African Association (AA).

1950 Abdul Sykes na Dr. Vedasto Kyaruzi wakachukua uongozi wa TAA na katika mabadiliko makubwa waliyofanya ni kuunda TAA Political Subcommittee.

Wajumbe wa kamati hii walikuwa: Dr. Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, John Rupia na Steven Mhando.

Kamati hii ndiyo iliweka mipango ya kuunda TANU kiongozi akiwa Abdul Sykes na Hamza Mwapachu.

Ni historia ndefu lakini unaweza kuipata hapa: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

Screenshot_20210817-065227_Photos.jpg


IMG-20210816-WA0141.jpg
 
Back
Top Bottom