Jifunze jinsi ya kufanya Usafi wa Maliwatoni

Jifunze jinsi ya kufanya Usafi wa Maliwatoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
pink-bathroom.jpg


Maliwato (choo na bafu) ni sehemu muhimu sana katika nyumba na ni sehemu inayohitaji usafi wa hali ya juu sana. Mara nyingi maliwato hujengwa kwa vifaa ambavyo ni rahisi kusafisha (tiles). Kama utakuwa na utaratibu wa kila mara mtu anapotumia bafu basi kuhakikisha ameondoa sabuni yote iliyorukia ukutani (kwenye tiles) kwa kumwagia maji basi usafi wa bafu hautakuwa kazi ngumu.

Ni vyema bafu na choo vikasafiswa kila siku na angalau mara mbili kwa wiki ufanyike usafi mkubwa wa kusugua kila sehemu ya choo na bafu kwa sabuni na dawa maalumu za kusafishia maliwato.

Kwa bafu kwanza safisha sinki la kunawia na kioo (kama vipo) kwa sabuni maalumu ya kuua vijidudu na brash maalumu kisha suuza kwa maji safi. Halafu safisha bomba zote kwa brash au sponge maalumu na ukimaliza anza kusugua tiles (kuta) na sakafu kwa sabuni na brashi.

Hakikisha umesugua kabisa hasa kwenye muunganiko wa tile moja na nyingine na kwenye kona za bafu. Usiwe na haraka bali hakikisha umesugua kila sehemu kwa ufasaha. Kama kuna bath tube basi lisugue pia kwa sabuni na brash ndani na nje hadi liwe safi kabisa. Sakafu ya bafu isiposuguliwa vizuri husababisha utelezi na ni hatari kwa watumiaji wa bafu.

Kwa choo kwanza chukua dawa/ sabuni ya kusafishia choo na imwagie ndani ya choo kwenye sehemu yote nyeupe kisha iache kwa muda wa robo saa. Baada ya muda huo kuisha chukua brashi safi ya kusugulia choo na sugua kwa ndani ya choo hadi uchafu wote uondoke na kuwa cheupe kabisa kisha chukua brash nyingine na sugua sehemu ya kukalia na pembeni (kama ni cha kukaa) na kwenye tanki la maji kisha suuza kwa maji safi na kusafisha brash yako.

Ukimaliza safisha dirisha na kisha kuta na sakafu. Baada ya kumaliza usafi hakikisha brashi zote ni safi na acha mlango na dirisha wazi kwa muda ili hewa safi iweze kuingia. Waweza weka ‘air freshner’ ili kuleta harufu nzuri maliwatoni.


Ubarikiwe na Bwana Yesu!


womenofchrist
 
Moja ya nyuzi bora zaidi JF japo,pongezi sana kwa kutukumbusha majukumu yatu maana wengi wanapakimbia chooni mpaka wabanwe na haja ndio wanapakumbuka,kuna nyumba ukienda jisaidia hata kuchutama tu unaona kinyaa
 
Moja ya nyuzi bora zaidi JF japo,pongezi sana kwa kutukumbusha majukumu yatu maana wengi wanapakimbia chooni mpaka wabanwe na haja ndio wanapakumbuka,kuna nyumba ukienda jisaidia hata kuchutama tu unaona kinyaa
Heh! We mpk utie jungu ndiyo unaona umeongea point
 
Nzuri zako zote huwa nazipenda .mbali na kuelimisha zinanifanya nizidi kuamin bado kuna wanawake wanaostahili kua wake zawatu.
 
Back
Top Bottom