Jifunze kanuni chache anazotumia Bilionea Elon Musk kuendesha makapuni yake 7 kwa wakati mmoja na yote yanafanya vizuri Duniani

Jifunze kanuni chache anazotumia Bilionea Elon Musk kuendesha makapuni yake 7 kwa wakati mmoja na yote yanafanya vizuri Duniani

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Bilionea Elon Musk anaendesha makampuni yake 7 Duniani kwa wakati mmoja na makapuni yote yanafanya vizuri Duniani.

Elon Musk ni muanzilishi, mkurugenzi na mmiliki wa makampuni 7, SpaceX, Starlink, X(Twitter), X Artificial intelligence, Boring Company, Tesla na Neuralink. Makampuni yote haya Musk anayendesha kila siku, yaani yeye ndio mkurugenzi mtendaji na muendeshaji wake kila siku.

Hivi hapa ni kanuni chache za Elon anazotumi kuendesha makapuni yake 6 kwa wakati mmoja.

1. Elon hapendi vikao visivyo na kichwa wala miguu, anasema vikao viwe vile tu vya lazima na visizidi nusu saa.

2. Elon anasema watu wakaimishe kazi, sio kila kazi ufanye wewe kwa kua wewe ndio boss basi unaamini kazi ukiifanya wewe ndio itakua nzuri ama wewe ndio unajua sana kwa kua wewe ni boss.

3. Kasi, Elon anapenda kwenda na kadi na muda. Elon aliwahi kufanya kazi ambayo ilikua inahitaji miezi 6 kwa siku 6. Speed is everything. The tighter the deadline the more work get done in a shorter time.

4. Uwajibikaji yeye anatambua aliefanya kazi na sio boss. Kama kazi imefanywa na engineer flani ama mfanyakazi flani, yeye anamtambua huyo mfanyakazi moja kwa moja badala ya boss iuchukua sifa zote, yeye hutambua mchango wa aliefanya ile kazi. Elon anasema ukimtambua yule mfanyakazi moja kwa moja inaongeza hamasa ya kufanya kazi.

5. Elon hapendi kufanya kazi kwa kufuata line of command, anasema kufanya kazi kwa kufuata mlolongo wa kiutawala unachelewesha kazi. Mfano ofisa w chini aanze kwa supervisor wake, supervisor aende kwa manager wake, manager aende kwa senior manager, senior manager aende kwa director, director aende kwa vice president ama deputy managing Director. Taarifa kutoka kwa MD itafuata mlolongo huo huo sasa anasema hii inapoteza muda, kama MD anamjua mtu flani anafanya kazi nzuri mpigie mmoja kwa moja muagize afanye hiyo kazi haraka na kama afisa wa chini unajambo unataka kuongea na MD nenda moja kwa moja hakuna kupitia mlolongo.

Soma hapa maelekezo ya Elon kwa wafanyakazi wa Tesla.
20240923_200343.png
 
Watanzania wengi ni mazuzu, hawajui umuhimu wa muda, ni wezi wanakuibia tajiri na ni wachawi wanatamani ufilisike wakucheke. Pia hawana ubobevu na ufanisi kazini. MTU anafanya KAZI hiyohiyo miaka mitano, lakini hamna ongezeko la ubora wa KAZI yake. Inaumiza sana
 
Wabongo wanafanya kazi kwa mazoeya sio kwa ufanisi .
1-Akiingia kazini tu kwanza anataka umbeya wa kila jambo .Saa moja kaua.
2-Anataka kujua mambo ya mpira au muziki. Saa mbili kaua.
3-Ataangalia kazi kdg kama lisaa tu tayari saa 3
4-Anatoka kwenda kunywa chai saa 3 mpk saa 4.
5-Anamaliza kunywa chai anakwenda chooni nusu saa.
6-Saa 4 ndio anaanza kufanya kazi mpk saa 7 lunch time.
Almuhimu mbwembwe ni nyingi kuliko ufanisi wa kazi yake hajali kama kuna wateja wanataka kuhudumiwa ndio maana hutokea mmoja wa wafanya akawa star huo anapiga kazi kishenzi wateja wote huyo ndio suluhisho lao , siku akiwa off wataja wote wanamuuliza huyo.
 
Hatari sana mkuu.
 
Hiyo nilikutana nayo nikiwa mtumishi wa Tanesco pale Mikocheni style na mfumo wa kazi ni wa ajabu, na hiyo nadhani ni mpaka leo ....
Muda wa kujipanga ili mkafanye kazi unazidi muda wa kazi yenyewe....
Ni shida....
 
Tunamengi ya kujifunza kwake. Yuko bize lakini anafuatilia karibu kila kitu duniani.
 
Hiyo nilikutana nayo nikiwa mtumishi wa Tanesco pale Mikocheni style na mfumo wa kazi ni wa ajabu, na hiyo nadhani ni mpaka leo ....
Muda wa kujipanga ili mkafanye kazi unazidi muda wa kazi yenyewe....
Ni shida....
Ndio maana wakisikia kuna ubinafshaji wanachanganyikiwa.... ninavyoyajua mashirika mengi ya umma, wanaofanya kazi inawezekana ni 30% tu; wengine ni mizigo tu.
 
Virtual Money......yeye anaangalia tu computer wanaosimamia ni wengi
Unakuta mtu ana duka la mpesa/wakala na pembeni anauza gesi akili inachemka balaa. Ukimuita huku anasema subiri unanichanganya. Elon Musk anaendesha makampuni 7 makubwa Duniani.
 
Ndio maana wakisikia kuna ubinafshaji wanachanganyikiwa.... ninavyoyajua mashirika mengi ya umma, wanaofanya kazi inawezekana ni 30% tu; wengine ni mizigo tu.
Ni kweli, ruhusa na udhulu usio na maana kila siku.

Ktk wiki siku za kazi ni sita ila wanafanya siku tatu. Akijitahidi ni Nne. Tena akiwa boss ndio usiseme anakuja kazini muda anaotaka na kuondoka muda wowote.
 
Nikifungua kampuni yangu fulani basi nitatumia hizi kanuni
 
Elon anajituma sana, lakini hiyo formula yake kui apply kwa hapa kwetu bongo! uongo.
 
Back
Top Bottom