Jifunze kidogo toka maktaba ya UVIMO

Jifunze kidogo toka maktaba ya UVIMO

frabel

Member
Joined
Mar 13, 2021
Posts
96
Reaction score
60
Uvimo Maktaba.

Uvimo Civil Group tukiwa wazoefu na watoa huduma kuanzia

  • Kuchora ramani
  • Kusoma ramani
  • Kujenga kwa au bila ramani
  • Kupaua
  • Plasta
  • Bomba plumbing
  • Uwekaji umeme wa kisasa
  • Rangi
  • Tiles
  • Brandering na kufunga bodi
  • Kuweka gata/kinga maji.
  • Kutengeneza jikoni.

Sasa Maktaba yetu leo hii itaangazia Mlinganyo wa gredi ya saruji, aina ya mchanga na aina za maji kwa ajili ya plasta na vigae.

Uvimo tumeendelea kutoa elimu na kujadilisha mada mbalimbali, adhma yetu kuu tukiwa kama wataalam tulio wekeza kwenye tasnia ya ujenzi na makazi ni kusaidia wadau wa ujenzi kuepuka au kupunguza hasara zitokanazo na mafundi wasio wataalam wasababishao hasara. _ Hata hivyo sisi pia tunafanya kwa vitendo kusaidia

Kimsingi[emoji1427] tuangalie resho na aina za

1-Sement
Si kila mfuko wa sement una resho sawa na mingine kwa sababu

i-Sementi #32.5
Hi ni gredi ya chini, ina gundi kidogo resho yake inatofautiana na 42.5

ii-Sementi #42.5
Hii gredi ya juu ,ina gundi nyingi, resho yake na mchanga ni kubwa.
Hata hivyo aina zote hutegemea aina ya kazi na imetoka kampuni gani.

2-Mchanga

Mchanga hutofautiana na kutegemeana na mahali ulipo chukuliwa.

i-Mchanga wa mtoni.
Sifa kuu ya mchanga wa mitoni au barabarani ni ukubwa wa punje zake.
Resho yake ni tofauti na ile ya (ii[emoji1427])

ii- Mchanga wa nchi kavu bila chumvi.
Sifa kuu ni punje ndogondogo.
Resho yake nitofauti na (i-[emoji1369][emoji1427])

iii- Mchanga wa nchi kavu asili ya chumvi.
Resho yake nitofauti na (iⅈ-[emoji1369])
Kwa ujumla wake aina ya mchanga na mlinganyo una mchango wa kumomonyoka kwa plasta na vigae

3-Aina za maji
i-Maji ya chumvi.
Yana uwezo mkubwa wa kukata nguvu ya sement.
Mlinganyo wake ni tofauti na (ii[emoji1427]) kutokana na pH ya maji haya ni ndogo sana, inapo kutana na saruji huleta madhara.

ii-Maji baridi/portable water.
Hayana chumvi na hutumika kwa shughuli zote za kijamii.
pH yake ni kubwa kiasi cha kutovunja nguvu ya sement.

Kimsingi injia au fundie wako anapashwa kutambua haya kabla ya kuanza kazi. Vinginevyo utapata shida siku za usoni.

Hata hivyo kwetu Uvimo, resho zote huzingatia sababu 3 hapo juu ili kuwa na nyumba madhubuti.

Ili kuepuka matapeli yanayo tumia jina la UVIMO kuharibu , Maktaba yetu inakukumbusha kuwa, namba za ofisi zetu ni

0629361896 -Kupiga
0753927572 -WhatsApp

Aksante.
 
Back
Top Bottom