Jifunze Kiingereza kizuri kabisa kutoka kwa Umoja wa Yanga WhatsApp Tanzania

Jifunze Kiingereza kizuri kabisa kutoka kwa Umoja wa Yanga WhatsApp Tanzania

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Katika kuonyesha kwamba hawajawaachia tu Wadau wakuu wa Elimu nchini Tanzania ambao ni Waziri husika wa Elimu, Walimu wote wa Somo la Kiingereza nchini Tanzania pamoja na Mwalimu anayekuja kwa kasi katika ufundishaji wa Somo rahisi kwa wenye nia ila gumu kwa Watanzania hasa Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Klabu Yanga leo Umoja wa wana Yanga wa Kundi la WhatsApp umeamua kutoa Mafunzo ya bure kwa wale wote wasiojua ama kusoma au kuandika vizuri Kiingereza.

Kwa kuanzia tu na Somo la awali Umoja huo wa Kundi la Yanga WhatsApp leo umeanza na Somo maalum la kutafsiri maneno ya Kiswahili kwa lugha ya Kiingereza ambapo walianza hasa na maneno haya ambayo yap / yanapatikana pia katika Kurasa yao ya Yanga WhatsApp hivyo Wewe usiyejua vizuri Kiingereza unaweza ukapitia ili nawe uweze kuwa vizuri katika hiyo lugha uweze kuungana na Yanga wa Kimataifa.

Kiswahili cha Yanga WhatsApp

Klabu ya Yanga leo imeendelea na mazoezi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam kujiandaa na mchezo wa raundi ya 6 dhidi ya Kagera Sugar

Tafsiri ya Kiingereza kwa sentensi hiyo ya juu kutoka kwa Yanga WhatsApp ni kama ifuatavyo

For Yanga Club today has continued with the practice in the field of Freedom in Dar Es Salaam to prepare the game round 6 against Kagera Sugar.

Nimalizie tu kwa kuwapa pole sana TFF ( Shirikisho la Soka Tanzania ) hasa baada ya wao kusakamwa kwa kitendo cha kuandika vibaya neno katika ile Ngao ya Jamii ambayo Klabu bora kabisa barani Afrika kama si duniani ya Simba ililichukua kwani kumbe ni dhahiri kwamba matatizo haya ya hii Lugha ya Kiingereza yameanzia mbali hasa hasa katika Klabu ya Kimataifa kabisa ya Yanga.

Nawasilisha.
 
Siyo tu Ok lakini pia ujifunze vizuri hicho Kiingereza kwani Yanga WhatsApp hawataki ' masihara ' katika kushindana Kiingereza na Mwingereza mwenyewe ' Malkia '.
 
Siyo tu Ok lakini pia ujifunze vizuri hicho Kiingereza kwani Yanga WhatsApp hawataki ' masihara ' katika kushindana Kiingereza na Mwingereza mwenyewe ' Malkia '.
😀😀😀😀
 
Vipi mwalimu ras simba yupo huko??

Wewe umeshasikia Mtu anaitwa Ras Simba hivi unahitaji tena hapo Elimu yoyote ya Astashaha, Stashahada, Shahada , Shahada ya Uzamili au Shahada ya Uzamivu kujua kwamba ni mwana Simba Sports Club mwenzetu tena wa Kindakindaki Mkuu? Simba SC haina ' wapuuzi / hopeless ' wengi kama wale wanaopatikana katika Klabu ya Yanga.
 
Simba mnawashwa sana, subiri tutawakuna kiwanjani..
 
Nyakati hizi wenzetu wanafuzu kombe la dunia sisi tunakosoana kuandika kiingereza! Kina Costarica, Brazil, Ujerumani hawana mpango na hiyo lugha lakin wameshafuzu fainali za kombe la dunia! Tutaendelea kushindwa siku zote kama wadau wa soka tutajikita kujadili vitu vidogo kama hivi sijui vya kuandika kiiengereza!
 
Umemaliza kila.kitu mkuu

Asante
 
Back
Top Bottom