Jifunze kilimo cha nyanya

Mkuu huu ugonjwa uliwahi nipata nilipulizia innovex ukaisha kabisa
 
Mkuu nimefanikiwa kufanya hilo zoezi na nilichoelewa ni kwamba kuna bacterial wilt.

Tazama picha

View attachment 706517
Nasubiri muongozo wako juu ya tiba
Nahisi nimechelewa sana kujibu hili ilaa itasaidia wengine
Jitahidi sana kulima mbegu yenye ukinzani wa huu ugonjwa na kama umeona dalili shambani ng'oa Miche iliyoathirika then piga dawa INNOVEX Kwa dosage ya 30 ml per 20 litres ya maji changanya na ridomil gold au fungicide yenye kiambato Cha mancozeb na cymoxonil 60 gram piga Kwa pamoja tatizo litakwisha kabisa.
 
Shida ya nyanya kupasuka kipindi mvua zikiwa nyingi mfululizo kama hizi za elnino husababishwa na mini wataalam

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile app
 
Shida ya nyanya kupasuka kipindi mvua zikiwa nyingi mfululizo kama hizi za elnino husababishwa na mini wataalam

Sent from my TECNO W2 using JamiiForums mobile
Majii yanakua mengi mno wakati nyanya ikiwa imekuzwa Kwa unyevu kidogo then maji yakaongezeka ghafla nyanya inaongeza ukubwa wa tunda wakati ganda la nje ni dogo ndipo hupelekea nyanya kupasuka.

Ushauri:
Kama umelima nyanya na unaona itakutwa na mvua jitahidi umwagilie maji mengi mara Kwa mara ili izoee Incase mvua itakuja itasaidia kupunguza tatizo na pia
NB
weka mbolea yenye calcium Kwa wingi.
 
 
Hii inasababishwa na nini wakuu
 

Attachments

  • IMG-20241127-WA0021.jpg
    178.3 KB · Views: 3
Hii inasababishwa na nini wakuu
Bilà shaka huu ni mnyauko, miziz huanza kukauka so maji na virutubisho vinashindwa kupanda juu hivyo hupelekea mmea kunyauka na hatimaye kufa ata kama una matunda. Hii ni miongoni mwa magonjwa yanayosababishwa na udongo, jaribu kumuona mtaalamu wa kilimo atakupa ABC about it..
 
Shukrani sana mkubwa
 
Hapa kuna Calcium deficiency ama Kutokana na Joto, umwagiliaji wako wa maji haujaMeet demand ya Miche yako, Hivyo, Jitahidi kwenye routine ya maji lakini pia Piga mbolea ya juu ambayo ni rich in micro elements particularly Calcium kama Wuxal ambayo ni excellent sana. Na mbolea ya chini tumia CAN, au ukipata Yara Minner ni super zaidi.
 
Mkuu hivi kuna mbolea ya maji ya kukuza mmea na ya kuzalisha?
 
Mkuu hivi kuna mbolea ya maji ya kukuza mmea na ya kuzalisha?
Ndio mkuu, zipo nyingi kutoka makampuni tofauti. Mf. Busta zote ni mbolea za juu(fortified liquid fertilisers) na hutofautiana pia ubora. Tumia wuxal, Tanzanite, supergro, Vegimax. Au rich in calcium mf. Calcium match
 
Ndio mkuu, zipo nyingi kutoka makampuni tofauti. Mf. Busta zote ni mbolea za juu(fortified liquid fertilisers) na hutofautiana pia ubora. Tumia wuxal, Tanzanite, supergro, Vegimax. Au rich in calcium mf. Calcium match
Shukrani mkuu...ila lengo langu nitumie mbolea za maji kwenye kilimo cha ufuta sasa kuna mtu alinieleza kuwa hizi mbolea za maji zipo za kupandia,kukuzia na kuzalisha hivi je kuna ukweli wowote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…