Jifunze kuhusu dhamana za fedha(financial securities)

Financial Analyst

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
1,849
Reaction score
3,506
Financial securities (Financial instrument/Financial asset) au Dhamana ya fedha ni mikataba ya fedha yenye thamani ya pesa na yenye uwezo wa kuuzika kati ya washirika wawili. Inaweza kuwa fedha, ushahidi wa maslahi na umiliki katika chombo (ushiriki), au haki ya mkataba wa kupokea au kutoa fedha.

-inaweza kuwa kati ya mtu mmoja na chombo cha fedha, mashirika ya baishara, serikali au kampuni.

-inaweza kuwa kati ya kampuni na kampuni nyingine, serikali, chombo cha fedha au mashirika ya biashara.

AINA ZA DHAMANA YA KIFEDHA
Hizi zimegawanyika katika makundi matatu:

1: EQUITY SECURITIES (HISA)
-Hii inamaanisha dhamana inayokuwezesha kupata umiliki wa sehemu ya kampuni, taasisi au shirika.
Makampuni yanatoa na kuuza hisa, then waweza kununua hisa kadhaa ili uwe sehemu ya umiliki na kuweza kupokea mapato kila mwaka wa mapato wa kampuni.
-Aina ya hisa inayotumika hapa ni Common stock, hii inakuruhusu kuwa na nguvu ya kura ndani ya shirika ila mapato yanapokuwa chini inakubidi na wewe upokee mgawanyo wa chini.

2: DEBT SECURITIES (DHAMANA YA MADENI)
-Hii ni dhamana inayoweza kununuliwa au kuuzwa kati ya pande mbili na ina masharti ya msingi , kama vile kiasi kilicho kopwa, kiwango cha riba, na ukomavu(maturity). Ni wajibu ambao unawezesha shirika au serikali kutafuta fedha na kuahidi kulipa wakopeshaji kwa mujibu wa masharti ya mkataba.

Aina za dhamana za madeni;

a) Government bond (dhamana ya serikali)
-unaweza kununua dhamana ya serikali kwa kuikopesha serikali kiasi kadhaa katika muda muafaka (miaka 5 hadi 20) na serikali ikawa inakulipa riba kwa nyakati m hadi pale mkataba utapokomaa na pia kukurudishia kiasi ulichokopesha serikali.

b) Corporate bond (dhamna ya mashirika)
-unaweza kununua dhamana ya shirika kwa kuikopesha serikali kiasi kadhaa katika muda muafaka (miaka 5 hadi 20) na shirika ikawa inakulipa riba kwa nyakati m hadi pale mkataba utapokomaa na pia kukurudishia kiasi ulichokopesha shirika.

c)Preffered Stock
-Hii ni aina hisa ambayo unakuwa unalipwa katika kiwango maalum na kisichobadirika na ulipwaji katika nyakati zisizobadirika. Unaweza kuinunua katika mashirika na kupata mgawanyo kabla ya wanahisa wengine, shirika likilfilisika wewe ndio unalipwa wa kwanza baada ya wamiliki wa juu lakini unakuwa hauna nguvu ya kura katika shirika.

d) Fixed deposit
Unaweza ukawekeza pesa zako katika akaunti ya kibenki au shirika la kifedha, akaunti ambayo hautaweza kuitoa pesa kwa muda maalumu utakao kubaliana na shirika la kifedha na utaweza kupokea riba ya juu kutoka kwa benki.

e)Mortgage
-Hii ni dhamana ya mali isiyohamishika, Anayeazimwa ana wajibu wa kulipa katika nyakati maalum na tofaut zilizokubaliana katika mkataba.Hii hutumiwa na watu binafsi na biashara kwa kufanya manunuzi ya majumba, viwanja n.k na mali zisizohamishika bila kulipa bei yote mali isiyohamishika.


3: DERIVATIVE SECURITIES
-Hizi ni dhamana ambazo thamani yake inategemea thamani ya dhamana nyingine nyingine. Derivative ni mkataba kati ya pande mbili au zaidi, na bei yake inaathiriwa na kupanda na kushuka kwa mali/dhamana inayoiishikilia au kuiensesha hiyo derivative.

Aina za derivates;

a)Swap
Ni uwezo wa kubadirishana kati au baina ya dhamana na dhamana nyingine. Mfano unaweza kubadirisha bond dhidi ya hisa za preffered.

b)Option
Ni mkataba unaokupa haki (sio wajibu ) wa kuuza dhamana yako katika tarehe maalum na katika bei maalum kutegemea aina ya option.

c)Future contract
Ni mkataba kati ya mnunuzi na mnunuaji (ambao hawafamiani) kukubaliana bei , tarehe ya manunuzi hapo mbeleni.


ANGALIZO: Kumekuwa kuna Elimu ndogo juu ya dhamana za kifedha kwa sisi waTanzania. Matokeo yake foreigners na wawekezaji kutoka nje ya nchi ndio wamekuwa wakija kuzifanyia kazi vilivyo na kufaidika.

-Pata muda wa kuzifuatalia kwa kina na uchukue nafasi ya kuweza kuwekeza katika dhamana za kifedha ( Financial securities/ Financial Instruments/ Financia l Assets).


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nondo nzuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usichoke kuleta nondo nyingine (dhamana za Serikali na namna ya kununua)

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu
Vipi Unazimezea mate hizo dhamana?

Ukishazinunua tu,
Jiandae kiasikolojia kuishi kama SHETANI endapo kichaa kitampanda JIWE.

Unaitwa majina yote Mabaya, Kuanzia BEBERU, MPIGA DILI hadi KANGOMBA[emoji23][emoji41]



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaozijua wanasema hizo hazina hasara, ukiikopesha Serikali lazima itakulipa tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah..ni kweli ..dhamana ya serikali kama government bond yenyewe haina risk yoyote na effect yoyote ya kiuchumi either derpreciation, inflation..etc haziwezi kuaffect kiwango chako unachotakiwa kupata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: bbc
Yeah..ni kweli ..dhamana ya serikali kama government bond yenyewe haina risk yoyote na effect yoyote ya kiuchumi either derpreciation, inflation..etc haziwezi kuaffect kiwango chako unachotakiwa kupata.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mkuu kama uchumi utaporomoka? Nini madhara ya uwekezaji kwenye dhamana serikali za muda mrefu mfano bond ya miaka 20?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa mkuu kama uchumi utaporomoka? Nini madhara ya uwekezaji kwenye dhamana serikali za muda mrefu mfano bond ya miaka 20?

Sent using Jamii Forums mobile app
Bond za serikali zinachukuliwa kama safe investment, why? coz unapata FIXED INTEREST (riba isiyobadilik) haijaliishi purukushani za aina gani za uchumi.

Bond ni tofauti na uwekezaji wa dhamana nyingine, kwa dhamana nyingine kama shirika likifilisika.. ni rahisi kupoteza pesa na uwekezaji wako wa dhamana...ila kama serikali imeporomoka kifedha au kiuchumi (ambayo sio rahisi)...wale wanaoshikilia bond wanakuwa refunded mara moja... Ndio maana bond inaitwa "Risk-free"

Kitu amabacho kinachoaffect mwekezaji wa bond...ni inflation rates (mfumuko wa bei) na kupotea kwa thamani ya pesa. (Depreciation of money)

Kwa mfano, wewe interest unayopata kwa bond ni asilimia 8 kila mwezi..lets hyo asilimia nane ni Tsh 750,000.... So lets say , baada ya miaka minne uchumi umepitia mfumuko wa bei au/na kushuka thamani ya pesa ..hii haitabadilisha riba yako coz utaendelea kupata ile asilimia 8 ( Ths750,000) ...Ila kutokana na kushuka kwa thamni ya pesa baada ya miaka mitatu..ile Tsh 750,000 inaweza kuwa Tsh 748,500.

Lakini kama tena pesa iki appreciate (ongezeka thamani)..ile riba yako pia inaongezeka thamani yake.

Lakini haimaniishi kuporomoka kwa uchumi ..kunaangamiza uwekezaji wako wa bond na wewe kupata hasara. ....hapana!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi bondi tunanunulia wapi mkuu??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thanks mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi hv inahitajika pesa kiasi gani?cha uwekezaji katika hili ambao unaweza pata pesa inayo eleweka


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…