Jifunze kuishi na watu wa aina zote

Jifunze kuishi na watu wa aina zote

baba mausingizi

Senior Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
189
Reaction score
119
Kuna Story nimeikumbuka ya miaka Saba iliyopita.. Ngoja niihadithie kidogo iwepo hapa kama ukumbusho wa safari yangu mm na huyu Dada ex wangu popote alipo.

Anaitwa Teddy, nilikutana naye 2013 kanisani liitwalo KANISA LA YESU TANGA,( GLORY LAND CHURCH TANGA) Siku moja nilishinda naye ofcn kwangu, na nilikuwa busy kweli kweli, nakumbuka kesho yake tulikuwa tunasimamia harusi (wanakamati)

Tukiwa ofcn Mara usiku ukaingia, saa 1, saa 2, saa 3, saa 4, saa 5. Aisee hapa nilipo nacheka Huku na type... Teddy akaona Wala tu asife na maswali moyoni, akaniuliza hivi tunatoka saa ngapi hapa, nikamwambia kwa jinsi ninavyoona hapa saa 7 au saa 8 usiku ndio tunatoka. Nyieee Teddy 'alimaka' ( wondering)akasema huogopi? Hakuna wahuni huku,? Nikamwambia wapo lakini hakuna muhuni hata mmoja namuogopa zaidi Sana wao ndio waaniogopa.

Nifupishe, story.
Basi bhana ikafika mishale Kama ya saa 8 tenana madakika yake tukawatunatoka office, tunatembea kuelekea home, hatujapiga hatua nyingi Sana yaan Kama vichochoro viwili saa ngapi tusikutane na wahuni nyie ngoje kwanza nicheke.

Teddy anajificha nyuma yangu, ananiambia tukimbie hapa manake Hawa mmmh hatutobozi, nikamwambia ngoja we subiri usiogope tunatoka hapa. Wale vijana walituzunguka, wakawa wanafanya Kama wanatusalimia, " oiii mambo,!" Tukaitika lkn Teddy moyo wake hupo.

Mara kidogo mmoja akanitambua, akamwambia wenzie oya huyo mwanaaa huyo. oyaa wawili wawascort mpaka huko mbele mbele,

Teddy aliona Kama Ni muujiza Basi ule ulikuwa mkubwa mno nakumbuka hatukulala usiku kucha Teddy ananiuliza mbona wametuacha, au na ww muhuni mwenzao nn.

Toka siku hiyo mpaka leo Teddy anajuaga mm na wahuni damu damu.

Nb, jifunze kuishi na watu wote kwa upendo, usibague kwa sababu ya kipato au tabia.. Hata ukiwaonesha upendo haimaanishi watakuambukiza tabia zao, may be wanaweza kubadilika kupitia wewe.. Wahuni nao ni binadamu tu kama ww. Malaya nao ni binadamu.

Acha kuishi vibaya na watu, bali weka alama nzuri kwenye mioyo yao ambayo itakulinda ww kila wakati
 
Back
Top Bottom