Jifunze kupuuzia

D Metakelfin

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
3,399
Reaction score
3,666
Kwenye MAISHA bila kujali wewe ni MWEMA kiasi gani ni lazima kuna watu ambao hawatakupenda, bila kujali umefanikiwa kiasi gani lazima kuna watu WATACHUKIA mafanikio yako, bila kujali unafanya nini kuna watu WATAKUSEMA VIBAYA. Hili ni jambo la kawaida sana.

Kitu ambacho watu waliofika juu huwa wanafanya ni kutumia Mkakati unaitwa "IF",yaani "IGNORE and FOCUS".Yaani huwa wanaamua kwa makusudi KUPUUZIA kila kisicho na Msingi na KUAMUA KUFANYA YALE ya MSINGI.

Ukweli ni kuwa hauwezi KUMRIDHISHA kila Mtu,Kadiri UNAVYOPANDA juu ndivyo WAKOSOAJI wako wataongezeka.Jifunze KUPUUZIA yasiyo na MAANA ili NGUVU YAKO isiishie KUBISHANA na KUWAJIBU watu bali ITUMIKE kufukuzia MALENGO YAKO.Pima kila jambo,kuna mambo ukianza kuyajibu ndio UNAYAPA NGUVU na UNAYAKUZA.

CHAGUA CHA KUJIBU,CHAGUA WA KUMJIBU,Sio KILA KITU na sio Kila MTU anastahili MUDA WAKO-Macho yapeleke Kwenye MALENGO YAKO.Kumbuka una MUDA mchache,Usikubali UPOTEZEWE Muda na WATU ambao WAMESHAPOTEZA mwelekeo.

See You At The Top

[HASHTAG]#TIMIZAMALENGOYAKO[/HASHTAG]
 
Nzuri hiyo
 
ngoja ni IF huu uz

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
HIS IMPERIAL MAJESTY EMPEROR HAILE SELASSIE I THE FIRST-DEFENDER OF THE FAITH.

Uko sawa m Cush

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…