Beeb
JF-Expert Member
- Aug 18, 2018
- 29,394
- 59,069
Habari zenu wapendwa? Naamini wote mko poa.
yna2 Leo nimeamua kuwaletea somo la namna ya kutengeneza mafuta ya kujaza ndefu kwa wanaume (natural beard balm).Mafuta haya siyo kwamba yatajaza ndevu tu ila yanatafanya ndevu na mn'garo,kuondoa mfungamano,na kuondoa m'ba.
MAHITAJI
Beeswax (sega la nyuki) 1tbsp
- Kazi yake ni kufanya mafuta yetu yagande na vilevile inasaidia kufanya nywele in'gae.
Shearbutter 1tbsp
- Inauwezo wa kujaza nywele na kuipa ulaini na mn'gao.
Coconut oil 2tbsp
- Kazi yake kujaza nywele na kuondoa ukavu kwenye ngozi na kuifanya nywele in'gae (nakushauri tumia mafuta ya Nazi yasiyopikwa)
Sweetalmond oil 2tbsp
- Kazi yake kuzuia nywele isikatike,kuipa nywele mn'gao,na kuijaza.
Lavender essential oil 10drops
- Kazi yake kuondoa matatizo ya ngozi Kama m'ba..fangasi kwenye ngozi..kuzuia nywele kukatika na kujaza nywele.
Rosemary essential oil 5drops
- Kazi yake ni kuifanya nywele kua nzito..ndefu.. kupunguza wingi wa mafuta..kuipa nywele ulaini na mn'gao.
JINSI YA KUTENGENEZA
Weka sufuria jikoni ..weka maji yachemke ..chukua sufuria nyingine au bakuli la udongo weka beeswax na shearbutter..chukua bakuli lako/sufuria weka juu ya sufuria lenye maji huku ukikoroga taratibu hadi iyeyuke.
Kwanini tunayeyusha butter na beeswax juu ya sufuria nyingine badala ya kuiweka sufuria moja kwa moja kwenye Moto? Tunafanya hivi sababu ya kuepuka kuua vitamini zilizomo kwenye butter na beeswax.
Butter na beeswax vikiwa vimeyeyuka weka mafuta yaliyosalia isipokua essential oils..koroga Kisha ipua.
Acha yapoe kidogo weka essential oils..koroga vizuri Kisha weka kwenye vikopo tayari kwa kuuza/kutumia.
Nb: ukikosa Sweet Almond oil tumia castor oil sio yale ya rangi nyeusi.
Ahsanteni.
Mchana mwema.
Michango ya wadau

----Hizo hapo ni baadhi ya bidhaa za matunzo ya ndevu. Binafsi hizo ndo ninazozitumia kwa sasa.
Hapo beard wash za aina mbili. Hizi ni shampoo ambazo ni mahsusi kwa ndevu.
Pia ndevu zaweza kupakwa mafuta. Kwenye picha utaona Cantu Shea Butter beard oil. Ni mafuta bomba sana kwa ndevu.
Muhimu vilevile ni ndevu kuzitunza mara kwa mara kwa sababu ni nywele ziotazo haraka sana [kama unazo nyingi].
Kwenye picha utaona wembe utumikao kuzichonga ndevu ili ziwe na muonekano maridadi.
Ndevu pia huchanwa. Hapo utaona kuna brush ya kuchania ndevu.
Hakika ndevu zikitunzwa, huwa zinaonekana vizuri mno.
View attachment 1251561
-----Binadamu tunahangaika sana,kipindi cha nyuma kila mtu alikuwa anahangaika kunyoa ndevu mpaka wengine wanaota mapele zikawa zinauzwa cream za kutoa ndevu bila kunyoa,sasa hivi fashion ya kufuga ndevu naona ndio inayo trend zimekuja dawa za kujaza ndevu,this world is moving too fast...
Hizi product zinapatikana huku kwetu kwa mtogole kweli?
Kweli ndevu na kucha ni vitu vinakua sana, wengi tunapuuzia kutunza.
Inaonekana unazipa ndevu huduma ipasavyo mkuu. Keep it up bro