Jifunze kuweka Akiba

Jifunze kuweka Akiba

mjuba101

Senior Member
Joined
Oct 24, 2013
Posts
159
Reaction score
65
Jifunze kuweka Akiba

Unapozungumzia swala la hela ni lazima kila binadamu atahusika kwa namna moja au nyingine. Fedha ni moja ya vitu vinavyoamsha hisia za binadamu wote bila ya kujali umri, rangi, kabila wala dini. Fedha imepewa nafasi kubwa sana kwenye maisha ya kila siku ya binadamu.

Pamoja na kwamba fedha imepewa nafasi kubwa sana kwenye maisha ya binadamu, bado ndio kitu kinachomtesa sana binadamu. Watu wengi sana wanapitia matatizo mengi kutokana na fedha. Mtu anaweza kupata matatizo kwa kukosa fedha na pia mtu anaweza kupata matatizo makubwa kwa kuwa na fedha nyingi.



Kutokana na matatizo hayo fedha imepewa majina mengi, mazuri na mabaya. Na mara nyingi watu wamekuwa wanasema fedha ndio inaleta matatizo. Ila kiukweli fedha haina tatizo na mtu bali tabia zetu sisi binadamu kwenye mambo ya fedha ndio zinasababisha matatizo yote.(soma; tatizo sio fedha, tatizo ni wewe.)

Umekuwa ukisumbuka na fedha kila siku, unaona kipato hakikutoshi na hata kikiongezeka bado huoni mabadiliko. Unatamani sana uweke akiba ila unaona kipato chako hakitoshelezi wewe kujiwekea akiba hivyo kila mara unajikuta matumizi yako yanazidi mapato. Kama unapitia hayo ni kwa sababu kuna siri moja kuhusu malipo ambayo bado hujaijua. Leo utaijua siri hiyo na kama ukiamua kuitumia utabadili mfumo wako wa matumizi na utunzaji wa fedha.

Kipato chochote unachopata unamlipa kila mtu kasoro mtu mmoja muhimu sana. Unamlipa anayeuza chakula, unamlipa anayeuza maji, unamlipa anayeuza umeme, unamlipa anayeuza mafuta na wengine wengi.

Wote hao unawalipa kwa uaminifu mkubwa ili kupata huduma zao. Ila mtu ambae ni muhimu na ambae angetakiwa kuwa wa kwanza kulipwa unamsahau. Mtu huyo ni wewe. Ndio, mtu wa kwanza kulipwa ni wewe, yaani ni lazima uanze kujilipa.

Unajiuliza utajilipaje wakati hivyo unavyolipia ndio vya muhimu?

Katika kitabu cha MTU TAJIRI WA BABELI(the richest man in Babylon) imeshauriwa kwamba katika kipato chochote unachopata toa asilimia kumi ujilipe wewe kwanza. Asilimia hiyo kumi haitakiwi kuwekwa kwenye matumizi yoyote bali umejilipa wewe na inabidi kuitunza. Baada ya muda kiwango ulichohifadhi unaweza kuwekeza na kupata faida zaidi.

Unaweza kufikiri kwamba kwa kuwa kwa sasa una kipato kidogo basi huwezi kutoa hiyo asilimia kumi na kuweka pembeni. Lakini ukiangalia kwa kina ukiondoa asilimia kumi kwenye kiwango chochote cha hela hakuna upungufu mkubwa sana. Kwa mfano kwenye laki moja, asilimia kumi ni elfu kumi, na kama ukiiweka pembeni unabaki na elfu tisini. Kama utashindwa kutimiza mahitaji yako kwa elfu tisini hata kwa laki moja bado hutoweza kutimiza. Na kama utaona kuishi kwa hiyo asilimia tisini hakuwezekani basi ni vyema kufanya jitihada za kuongeza kipato chako.

Katika kipato chochote unachopata iwe ni mshahara au faida ya biashara hakikisha unaweka asilimia kumi pembeni. Fedha hiyo haitakiwi kuwa kwenye bajeti ya matumizi. Ni vyema ukajijengea utaratifu huu wa kuweka akiba kabla ya matumizi. Wengi wetu tumezoea kuweka akiba baada ya matumizi, na mara nyingi baada ya matumizi fedha yote inakuwa imeisha hivyo tunakosa cha kuweka akiba.

Anza sasa kujilipa kwa sababu wewe ni wa muhimu kwako zaidi ya hao wengine wote ambao unakimbilia kuwalipa kwanza. Unaweza kuweka akiba asilimia yoyote unayoona inafaa kwako ila isiwe chini ya asilimia kumi.

By Amani Makirita
http://amkamtanzania.blogspot.nl/p/pata-habari-kwa-email.html?m=1
 
Kitabu cha the ricest man in babylon ni kizuri but ninapingana nacho seemu moja.
Kuhusu kujilipa hiyo ni sawa lakini suala namba moja kabla ya kujilipa ni fungu la kumi.kwa kuweza kutoa fungu la kumi kwa Mungu wako its the better way to start with then percent nyingine kwa ajili ya akiba.
 
ahsante kwa ushauri.
Ngoja nianze kujilipa
 
Kwa kweli issue ya kujiwekea akiba, inahitaji somo la siku nzima na mwalimu aliyebobea...manake kwa wengi wetu ni msamiati....
 
No no . Ukisomemesha mtoto umeweka akiba, ukijenga nyumba ndiyo umeshaweka akiba. Ukianzisha mradi wa kudumu umeweka akiba. Ukimunua radii umeweka akiba, ukijenga guest umeweka Hakika, ukijenga shule umeweka akiba.

Kumbukeni pesa ushuka thamani kila kukicha so be careful. Left hamsini ya leo baada ya miaka kumi ni sh. Left mbili.
 
Back
Top Bottom