Jifunze kwa awa vijana wa kiafrika ni matajiri wabunifu umri wao chini ya miaka 30

GadoTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2014
Posts
370
Reaction score
636
Unaweza kujifunza kitu kwa awa vijana wenye umri chini ya miaka 30 lakini kwa ubunifu na juhudi zao wamefanikiwa kuwa matajiri.

LORNA RUTTO,Mkenya
Ana miaka 28 ndio mwanzilishi wa ECO POST, kampuni inayotengeneza nguzo za fensi kwa kutumia mabaki ya plastiki, ikiwa ni mbadala wa kutumia miti. Eco Post inakusanya mabaki ya plastiki na kutengeneza nguzo za kuweka fensi.

PATRICK NGOWI,Mtanzania
Ana miaka 28 ni mwanzilishi na mmiliki wa HELVETIC SOLAR CONTRACTORS. Ngowi alianz biashara akiwa na miaka 15 alipata mkopo kutoka kwa mama yake kwa ajili ya kuanzisha iyo biashara yake ambapo awali alianzia na biashara ya simu za kichina. Baadae aliamia kwenye hii biashara ya umeme wa jua haswa kwa maeneo ya kaskazini mwa Tanzania. Mwaka jana kamupuni ya Ngowi ilitengeneza dola za kimarekani millioni 3.

EVANS WADONGO, Mkenya
Wadongo ana miaka 26 alibuni taa ya kutumia chaji ya mwanga wa jua inayoitwa ‘MwangaBora’. Ubunifu wake ulisaidia kupunguza kero ya kutumuia vibatar
i na chemli za mafuta ya taa sehemu za vijijini mwa Kenya.

JOEL MWALE, Mkenya
Mwale ana miaka 20, anaendesha kampuni ya SKY DROP. Kampuni yake inazalisha maji ya kunywa yanayotokana na kukusanya maji ya mvua kuya-treat na kuuzwa kwa bei chee. Pia inazalisha na kusambaza bidhaa zinazotokana na maziwa.

OLUWASENU OSEWA,Mnaijeria
Mwanzilishi wa mtandao wa Nairaland. Nairaland ndio forum kubwa Africa yenye memba (Active members) zaidi ya milioni 1. Kwa Naijeria mtandao wa Nairaland inatembelewa na watu wengi kuliko ata Wikipedia.
 
Hizo takwimu wanachukulia wapi hapa Songea kuna kijana mmoja ana miaka 19 alipata madini aina ya saphire yenye thamani ya bilioni 200
 
Hizo takwimu wanachukulia wapi hapa Songea kuna kijana mmoja ana miaka 19 alipata madini aina ya saphire yenye thamani ya bilioni 200
mdau, awa vijana wametambuliwa na forbes 2014 ndipo nilipopata hizi taarifa zao na awa ni baadhi yao tu.
 
Hizo takwimu wanachukulia wapi hapa Songea kuna kijana mmoja ana miaka 19 alipata madini aina ya saphire yenye thamani ya bilioni 200

Watu wanaongelea waanzilishi wa makampuni yenye kazi tofauti, wewe unaongela "alipata madini". Wapi na wapi?

Billion 200 unazijuwa zilivyo au unajisemea tu?

Hizi shule huwa mnaenda kusomea ujinga?
 
Sasa wewe!, kwani ukimchukia tajiri ndio itakupunguzia njaa au?!!. Huyu ni mtanzania, tujifunze pia kwake. Ni jinsi gani katoboza katika mazingira hayahaya ya kishenzi. Sio kutwa kijicho tu. Chukua hiyo wewe boy.a.

Wakiletewa Vijana waliotoboa kwa jasho wanalalamika...
 
Watu wanaongelea waanzilishi wa makampuni yenye kazi tofauti, wewe unaongela "alipata madini". Wapi na wapi?

Billion 200 unazijuwa zilivyo au unajisemea tu?

Hizi shule huwa mnaenda kusomea ujinga?

Kwa leo nimekupa like, huyo jamaa ni anakurupuka tu kama mtu aliyefumaniwa, kama hatumii kitu cha meru ni bahati sana:majani7:
 
Watu wanaongelea waanzilishi wa makampuni yenye kazi tofauti, wewe unaongela "alipata madini". Wapi na wapi?

Billion 200 unazijuwa zilivyo au unajisemea tu?

Hizi shule huwa mnaenda kusomea ujinga?

Kama ni waanzilishi wa makampuni mbona wako wengi sana lakini hawatajwi.? Nenda Brela uone kuna maelfu ya makampuni ya watu mbona hawatajwi anatajwa ngowi tu? Forbes wanamaanisha VIJANA WENYE PESA sio makampuni. Kuna kampuni nyingi tu zina mtaji hata milioni tano haifiki. We bibi unajifanya unajua kila kitu kumbe zuzu tu. Hiyo bilioni 200 kubwa kwako kwa wengine ni hela ya mboga tu
 
Mkuu laki si pesa kinachoongelewa hapa ni sustainable successes, hao jamaa wanaopata utajiri kupitia madini hasa kwa wale wanaoenda msumbiji mbona wapo wengi sana ila tatizo wengi wao pesa zinaisha kwa kukosa maarifa/ubunifu wa biashara endelevu.
 
Last edited by a moderator:
Watu wanaongelea waanzilishi wa makampuni yenye kazi tofauti, wewe unaongela "alipata madini". Wapi na wapi?

Billion 200 unazijuwa zilivyo au unajisemea tu?

Hizi shule huwa mnaenda kusomea ujinga?
Huyu ana shahada ya juu ya ujinga dada yangu,kaona tu jina kama la mchagga hapo kapandwa na maruhani.
 
Wewe ulikusudia kumtangaza Ngowi na si vinginevyo
Ujinga,umasikini na chuki ni kama vidole vya mkono mmoja,pigeni kitabu,pigeni kazi,punguzeni anasa mtafanikiwa tu,chuki na wivu havina faida yoyote kwenu.
Cc laki si pesa
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…