JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Ujasiriamali ni uwezo wa akili na ubunifu wa mtu kutambua fursa, kuiendea fursa, kuipangia mkakati fursa na hatimaye kuthubutu na kuiweka katika uhalisia yaani kuzalisha bidhaa yenyewe na mwisho kuitafutia soko na kuifanya itambulike na watumiaji.
Mjasiriamali anapaswa kufahamu kanuni mbalimbali ambazo zitamuongoza ili kuweza kufanya kazi yake kwa weledi, kanuni hizo ni:-
- Kuwa mtatuzi wa matatizo, mjasiriamali hutatua matatizo katika jamii na kisha kupata pesa kutoka kwa watu ambao umewatatulia tatizo husika.
- Kuwa na maono, maono ni kuona kile ambacho wengine hawakioni, hivyo mjasiriamali anatakiwa kuwa na maono na kuweza kuyabadili kuwa uhalisia.
- Chagua washirika au timu sahihi, endapo mjasiriamali utachagua washirika ambao siyo sahihi wanaweza kukwamisha maono yako.
- Toa huduma au bidhaa yenye tija.
- Fahamu na jali wateja, Mjasiriamali unapaswa kutambua kuwa unahitaji wateja kuliko wanavyokuhitaji.
- Tumia pesa vyema, matumizi sahihi ya pesa yatamsaidia Mjasiriamali kufikia malengo yake.Mjasiriamali ni vyema ajifunze kufahamu hii pesa ni ya nini na kuitumia ipasavyo.
- Usipuuze nafasi ya teknolojia, kupitia teknolojia kama vile simu na mtandao wa intaneti unaweza kufikia watu wengi zaidi na kuongeza mauzo ya bidhaa au huduma husika.
- Fahamu soko, ni muhimu kuhakikisha kuwa bidhaa yako inakidhi mahitaji ya soko lako.
- Jifunze kutoka na makosa, makosa hutoa somo muhimu sana kwa kila mtu hasa Mjasiriamali iwapo ulipata hasara kwenye biashara zako basi unaweza kujifunza kutorudia ulichokifanya awali ambacho kilikuletea hasara.
- Jifunze kwa waliofanikiwa, kama Mjasiriamali jifunze kuepuka ushauri wa watu ambao walishindwa kwa kuwa watu hawa wana maneno mengi hasa ya kukatisha tamaa kama vile ‘hili linahitaji pesa nyingi’ na ‘mimi lilinishinda’.
- Tumia muda vizuri, Mjasiriamali ni muhimu ukaondoa mambo yasiyokuwa na ulazima kwenye ratiba yako.
- Weka vipaombele, hii itakusaidia kufahamu kipi uanze kukifanya na kipi kifuate kulingana na umuhimu wake.
- Usikate tamaa, Mjasiriamali unaweza kukutana na changamoto mbalimbali hupaswi kukata tamaa muhimu kuweza kubadili changamoto kuwa fursa.
Upvote
3