Jifunze namna ya kuendesha boti ndogo

Jifunze namna ya kuendesha boti ndogo

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Jifunze kuendesha boti ndogo ambayo inatumia usukani (wheel) au ile ambayo hutashika ekseleta (throttle) iliyopo kwenye mkono uliunganishwa na engine.

Awali itabidi ujue namna gani ya kuwasha injini ya boti kama ni kutumia funguo au ya kuvuta kamba iliyopo katika engine.

Unapowasha injini hakikisha boti yako ipo ndani ya maji kwa kuwa injini hutumia maji ya ziwa/bahari kupooza.

1. Endapo boti yako ina usukani na kibadili gia na moto
Hizi ni boti zile za kisasa ambazo huwa na kibadili gia na moto. Unapowasha boti hakikisha vyote vipo sehemu ya katikati.

Baada ya kuwasha sogeza kifimbo cha gia sambamba na kifimbo cha moto kulingana na uelekeo unaotaka.

Mbele(Ahead) au nyuma( Astern). Unapotoka kama umeweka mbele ili kuongeza mwendo itakupasa uongeze moto zaidi ili upate kasi.

Upande wa kuongoza utatumia usukani mithili ya ule wa gari na kukata kona usizungushe kwa kasi mpaka mwisho ukiwa kwenye spidi kali hii itapelekea boti kuzunguka na utakosa control.

2. Boti yenye mkono wa ekseleta kwenye injini
Hizi ni zile injini ambazo zimepachikwa sehemu ya nyuma ya boti na muongozaji hukaa nyuma na huendesha kwa kutumia mkono uliotoka kwenye boti ambao una ekseleta na ndio hutumika kukata kona.

Boti hii huwashwa kwa kutumia njia ya kuvuta kamba kwa mkono( Kick Starter) baada ya kuiwasha kuna kifaa cha kubadili gia ambapo kuna mbele, neutral na nyuma.

Unapowasha hakikisha boti ipo neutral baada ya kuwaka weka gia na vuta mafuta taratibu kuondoka, utaongeza kasi kadri utavyoivuta ekseleta. Kukata kona utatumia huo mkono (handle) kupeleka kulia na kushoto.

Angalizo: Boti ikiwa kwenye maji ili ufanisi uwe mzuri inabidi propela inabidi izame kwenye maji.
Kwa boti za kawaida unapoifunga injini hakikisha umeinamisha kwenye maji(tilt) kadri ya uonavyo sahihi.

Kwa boti za kisasa zenye usukani kuna kitufe au remote utabonyeza kuinama ( tilt)mpaka angle unayoona ipo sahihi.

Wholesale-boat-accessories-boat-throttle-controller.jpg
images (1).jpeg
 
Back
Top Bottom