Jifunze namna ya kutumia Tsh 300,000 kama mtaji wa kufugia kuku

ASANTE MKUU KWA ELIMU YENYE MANUFAA
 
Mku As Salafiyyu91 hili ni somo zuri sana kiongozi, ila ingependeza kuanza na funzo la kupata hizo 300,000/=. Inaweza ikawa pesa ndogo kwa baadhi lakini kwa wengine ni kama kupanda mlima Kilimanjaro.
 
Hakuna uhalisia hapa kuna mambo mengi hayajaingizwa kwenye huo mchanganuo ambayo ni muhimu. Kuacha kujumuisha mambo yote kwenye mradi wa aina yoyote ile ni kutengeneza 'mama wa mabomu' ambalo litapelekea kuulipua mradi yaani kufa kwa mradi.
Huu mradi ni kama skeleton [emoji88], wewe jazia nyama na kwakuwa tayari umeshaona kasoro, zifanyie kazi. Hakuna mchanganuo ulio perfect kwa 100% na ndio maana wengi huweka pesa ya dharula pembani, ili endapo kitatokea chochote iwe rahisi kurekebisha
 
Mkuu kwa mfano mambo gani yamekosekana ?
Hoja ni nzuri na inahamasisha watu kuanzisha miradi midogo midogo isiyohitaji muda mwingi na mtaji mkubwa, lakini tukumbuke kuna vitu vingi sana ambavyo vinahitajika ili mradi uweze kustawi. Watu wananweza kuingia kichwa kichwa wakijua mambo ni mteremko, baadae wakapata hasara kumbe kuna mengi ambayo alikuwa hayajui.
Baadhi ya mambo yaliyorukwa ni kama ifuatavyo:-
1. Gharama za chanjo na madawa, ambacho ni kitu muhimu sana.
2. Gharama za nishati ya kuwakuzia vifaranga.
3. Gharama za kutengeneza/kununua vyombo vya chakula na maji kwa vifaranga na kuku wakubwa pia.
4. Gharama za ujenzi wa banda bora la vifaranga ili kuvilinda na wanyama na ndege waharibifu kama vile vicheche, paka shume, mbwa, mwewe, kunguru n.k.
5. Pia kuna variation ya bei za vyakula; vinapanda na kushuka kutokana na msimu. Mfano mwezi April 2017 Pumba ilipanda na kufikia Tsh. 40,000/= kwa gunia, Paraza ilikuwa ni Tsh. 1500 kwa Kg moja.
 
Ni mwangaza huu mengine tujiongeze kulingana na eneo utakalofugia changamoto hazifanani kwa kila sehemu.
 
Nimehamasika sana na biashara tatizo soko la uhakika la kuuzia hao kuku
 
Indeed
 
Kweli kabisa
 
Saaafi sana asante kwa mchanganuo uko vzuri sana
 
Hii ni idea nzuri sana. Ukiiboresha itakua poa tu.
 

Namshukuru sana mkuu, haya ndio mambo ya kushare.
 
Somo zuri, mimi nataka kujua hawa kuku tunaweza kuwapata wapi. Ni kuku wa kienyeji kabisa au ni chotara kama mdau mmoja aliesema hapo juu? Tunaomba majibu anaefahamu.
 
Mkuu kwangu tatizo ni banda nataka nifuge kuku ila wasiwe wa kutoka nje asa je gharama za banda zitakuwaje ndani ya 300000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…