Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 772
- 2,421
Nimeamka asubuhi leo na kukutana na threads kadhaa za watu wakilalamika kuhusu usaliti unaoendelea kwenye mahusiano yao. Na kwa miaka ya karibuni, 'uaminifu' kwenye mahusiano imekuwa ni kitu adimu sana na ukikipata basi ni bahati na itabidi upambane usikipoteze. Kila mtu ataongea mengi na atatoa ushauri wa kila aina ila uhalisia ni kuwa suluhisho pekee la hili janga ni kuipindua nature kitu ambacho HAKIWEZEKANI. Kama tungeweza kuipindua Nature, bila shaka usaliti ingebaki kuwa hisitoria. Ila sasa HATUWEZI.
Kwanini Nature?
Kwanini Nature?
- Wanaume asili yao ni kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja haijalishi ameoa au hajaoa. Ni rahisi sana kumkuta bikra chuo kikuu kuliko kumkuta mwanamme mwenye mwanamke mmoja...Hii ni nature na ndiyo inapelekea usaliti kwenye mahusiano..Unakuta mtu ameoa ila bado anamiliki hawara ambae ni mke wa mtu. Mpaka hapo usaliti unakuwa ni double at once.
- Binadamu tumeumbwa na matamanio. Hii ni nature, hakuna mwanaume au mwanamke asietamani. Na haya haya matamanio ndio yamekuwa yakipelekea usaliti katika mahusiano. Unaweza ukakuta mtu anapata kila kitu kwa mke/mme wake ila kwakuwa ameumbwa na matamanio, itamplekea kuingia katika uhusiano na mtu mwingine. Naomba hapa nitoe mfano kwa kumtumia member mmoja wa JF ambae alijikuta ammempenda Mjeshi kwa mara ya kwanza alipomuona. Siamini kama yule member hana Boyfriend, lazima atakuwa nae lakini nature ya matamanio tuliyoumbwa nayo inatufanya tusaliti watu wetu. Jaribu kufikiria kama yule member angebahatika kuipata namba ya yule mjeshi pale mlimani city, lazima usaliti ungetokea.
- Udhaifu wa kihisia. Hii ni nature ambayo inapelekea kutokea kwa usaliti kiasi kikubwa. Ndio maana Samsoni alimalizwa na Delila, ndio maana tunakumbushwa ngoswe penzi kitovu chauzembe. Ni rahisi kwa manamke kusimamia sheria kwa mwanamke mwenzie au mwanamme kwa mwanamme mwenzie kuliko mwanamke kusimamia sheria mbele ya mwanamme anaemvutia au mwanamme kusimamia sheria mbele ya binti mrembo.
- Tamaa. Binadamu tumeumbwa na tamaa. Hii ni nature pia. Hapa siongei sana maana kuna kitu kinaitwa PESA.
Sisi wote ni wasaliti hivyo usaliti hautakuja kuisha kamwe unless tuibadili nature kitu ambacho ni IMPOSSIBLE.
Nini kifanyike:
Kwakuwa hatuwezi kuishinda nature basi hatuna budi kuungana nayo. Badala ya kuwekeza nguvu na muda mwingi kumchunga mtu wako asikusaliti kitu ambacho hakiwezekani, ni bora ukatumia nguvu nyingi kujifunza mbinu ambazo zitakuepusha na maumivu ya usaliti ambao upo na tunaishi nao. Hizi mbinu zinategemea mtu na mtu kutokana na personalities zetu..Zifuatazo ni mbinu zangu ambazo huwa zinanifanya nisihisi usaliti kama nikiwana mtu ingawa najua upo..Yaani ni kama vile unajua kuna corona ila unajitahidi kuishi huku ukiidanganya akili yako hakuna corona:-
- Ukitaka kumla bata usimchunguze sana. Maswala ya kufatilia kila nyendo ya mtu wako na kufatilia kila simu inayoingia na kutoka utakuja kufa au kuua bure. As long as hakuoneshi usaliti waziwazi (anakuheshimu) haimaanishi kuwa ni mwaminifu. Basi usijikute commando au afisa kipenyo kufatilia nyendo zake utaumia bure siku moja maana waswahili hawakusema umzaniaye ndiye kumbe siye kwa bahati mbaya.
- Ni kweli wasiwasi ndio akili ila kuna muda wasiwasi na hofu ndio chanzo cha matatizo. Acha kuishi kwa hofu na wasiwasi. Namaanisha jukumu lako ni kuhakikisha mwenzi wako anafata misingi mliyowekeana..Kama kuja kwa wakati, kutimiza matakwa yote bila matatizo na kuheshimu mahusiano. Akishatimiza hayo basi kuwa na furaha na usiwe na wasiwasi wa kuanza kumchunguza sana bata mwisho usimle..Badala ya kutumia nguvu kubwa kumchunguza, tumia nguvu kubwa kumfanya azingatie katiba ya mahusiano yenu. Mengine yaache maana ni nature. Ila akivunja hiyo katiba ni ruksa kumuacha.
- Ni vigumu sisi kama binadamu kuwa waaminifu ila ni rahisi sana kuficha indicators za usaliti wetu kwa wenzi wetu. Kuna muda mpenzi anapigwa au anaachwa sio kwa sababu eti ni Msaliti maana hiyo ni nature haifutiki ila ni kwa sababu tu amekuwa mzembe kuficha ule usaliti wake.
Unaweza ukawa unamcheka mwenzio amesalitiwa bila kujua kuwa uliye nae ni msaliti wa kimataifa ila tu haonekani au hajioneshi. Mimi sihangaiki kutafuta mpenzi ambae sio msaliti (maana hayupo) ila nahangaika kutafuta mpenzi ambae atauficha usaliti wake nisiuone ambae huku jukwaani na duniani mnamuita mwaminifu.
Usaliti hautaisha kamwe kwasababu unasababishwa na nature na kwavile hatuwezi kuibadili basi yatupaswa kuungana nayo. If you can't fight them, Join them.
Usaliti hautaisha kamwe kwasababu unasababishwa na nature na kwavile hatuwezi kuibadili basi yatupaswa kuungana nayo. If you can't fight them, Join them.