Jifunze njia za uhakiki wa taarifa kubaini taarifa ya uongo

Jifunze njia za uhakiki wa taarifa kubaini taarifa ya uongo

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
IMG_20210401_100009_919.jpg
Nini maana ya uhakiki wa taarifa?

Uhakiki wa taarifa ni hatua zinazochukuliwa kwa lengo la kubaini taarifa ya uongo. Njia hii hutumiwa ili kupunguza ueneaji wa taarifa za uongo.

Kwanini uhakiki wa taarifa?

Uhakiki wa taarifa una umuhimu sana katika kipindi hiki cha dunia ya teknolojia iliyopelekea kukua kwa utengenezaji wa taarifa za kizushi na za uongo. Teknolojia imepelekea kwa sasa ni vigumu kutambua uzushi ni upi na uongo ni upi.

Uhakiki wa taarifa unasaidia kupunguza uwepo wa taarifa za uongo katika ulimwengu wa habari. Vilevile inasaidia kuondosha mitafaruku inayosababishwa na taarifa zisizo za ukweli katika jamii.

Namna ya kuhakiki taarifa mwenyewe;

•Angalia ni chombo gani cha habari kimetoa taarifa hiyo. Je, chombo hicho cha habari ni cha uhakika, kama una mashaka nacho basi uwe na mashaka na hiyo taarifa pia.

•Kama umeitilia mashaka taarifa fanya utafiti wako mwenyewe ili kujihakikishia. Unaweza jaribu kutafuta vyanzo vingine vinavyo aminika kuhakiki kama na wao wametoa taarifa hiyo.

•Tizama chanzo kilichotumika katika taarifa hiyo. Jihakikishie kama chanzo hicho ni cha kweli

•Angalia tarehe na muda wa taarifa hiyo. Muda mwingine taarifa zinaweza kuwa zinapotosha kupitia muda na tarehe.

• Mwisho kabisa ni vyema kuwa na utaratibu wa kuhakiki taarifa kupitia vyanzo mbalimbali vya habari, usitegemee chanzo kimoja tu.
 
Upvote 0
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom