Jihadhari na makampuni ya Kitanzania yanayoagiza magari

Sure boss.....
 
Kukikucha nitakupa feedback now ngoja nipumzishe fuvu....
 
Hongera kwa kuwasaidia watanzania wengi, hawa makanjanja wapo wengi mno.
 
Hongera kwa kuwasaidia watanzania wengi, hawa makanjanja wapo wengi mno.

Na hizi habari sambazeni na kwenye ma group ya whatsapp kwa wingi.

Sipendi dhuluma na uonevu. Kama ni Hela Mtu Atafute Ya Halali Sio Kuonea na Kudhulumu Wengine Plus ni mambo kama haya yanafanya hata wengine wanaofanya biashara hizi ki halali na wao waonekane sio wa kweli.

It Has To End.
 
Hapo kwenye whatsapp umenikumbusha njia nyingine wanayotumia. Huwa wanaunda na magroup ya whatsapp ukishalipia wana kuadd mule, sasa mule utakuta member kama 50 au zaidi hapo ujue kuna watu wao kama 15 hivi.... wanaanza kusifia kampuni kuwa jamaa ni wa uhakika mara tuliletewa gari and blaah blaah ili ku-win trust yako.... Ukijifanya una doubt huduma yao wataibuka watu kuwatetea kumbe ni wenzao.....

Jamaa wana mipango lukuki kupiga watu...
 
Nimepitia leo web yenu. Jana nilichanganywa na zile ads zinakuja kabla ya contents.

Pia naona forums nyingi hazijawa updated for more than a month.

Also majukwaa yamejificha sana mpaka uscroll kwenda chini ndio utaona forums mbalimbali.

Pia sijaelewa kwenye auction kuna kuweka 30,000 na ile 50,000 ina maana bid ikichukuliwa na mwingine hela inakuwa refunded?

Pia jitahidi iwe user friend kuaccess majukwaa like hapa JF ni easy majukwaa yapo juu tu ukitaka kuingia....

 
Sio kweli kabla ya makampuni twajwa hapo juu watu walikuwa wanunua wapi magari?
Tupe jina la kampuni inayoaminika na iliyoshika soko kuzidi kampuni tajwa hapo Juu,Hizo kampuni ni nadra kusikia malalamiko toka kwa wateja wao,hawana uhuni unaolalamikiwa na mtoa Mada,wana kasoro baadhi lakini ni zakuongeleka na za kurekebishika, Sio za kitapeli na Wizi (hawana)

Labda tutajie kampuni unayoifahamu yenye hadhi na heshima ambayo watanzania hatuijui,tusaidie.
 
Wewe umesema kiini cha tatizo hasa. Watanzania tuna akilifupi mno mno. Biashara karibu zote zimejaa ''ujanja ujanja'' na maneno mengi. Yaani mfanyabiashara haoni madhara ya kutokuwa mwaminifu hata kidogo. Ni tamaa mbele kwa mbele. Nadhani ni culture tuliyojenga kwa sababu ya uadimu wa bidhaa kipindi cha ujamaa. Muuzaji anakuwa ndiye mfalme na mnunuzi anakuwa kama mtumwa. Huwa nasema ombeni sana wachina wasije kuruhusiwa kufanya hizi biashara ndogo ndogo maana wabongo wote wenye biashara watakufa njaa.
 
Nia yako ni moja. Kutetea uozo unaosemwa hapa na pia kuwa-discourage watu wanaotaka kuagiza magari wenyewe kutoka Japan. Ni hivi: Mara nyingi ni salama zaidi mtu kuagiza gari mwenyewe kutoka Japan kuliko kutumia hizi kampuni za kibongo. Kama mtu yuko makini siyo rahisi kupigwa fedha kwani website za magari zinazoaminika zinafahamika na wengi ni waaminifu tofauti na wabongo wenye tamaa kama fisi.
 
Hivi huyu jamaa ameweza kuku-twist mpaka ukalainika? Unaona kweli hiyo link aliyoweka ni forum yenye hadhi ya kuaminika? Angalia usije kulizwa hapa. Tumieni website zinazoaminika ambazo umepewa link, hizo za Befoward na hiyo nyingine.
 
Hapo nyuma, nilishawishika kununua gari kupitia kwa wakala wa hapa Nyumbani.

Niliona Picha ya gari kupitia ukurasa wa Instagram, baada ya kuhoji gari la mwaka gani na limetembea Km ngapi, nilichojibiwa hakikuwa na uhalisia wowote.

Kwabahati nilipata website moja ya wauza magari kutoka Japan, Nikabahatika kukuta gari nililolihitaji kupitia kwa wakala yule wa hapa nchini, nakukuta taarifa alizonipa hazikuwa sahihi bali kuna mchezo alitaka kuucheza ili aje anihadae hapo baadae. Nilifanya maamuzi wa kutafuta gari lingine lenye vigezo ninalolihitaji na kulipia haraka.

Niliweza kupata gari zuri kwa gharama nafuu na kuepuka gharama kama ya T-sh 3m kama ningeamua kununua kupitia yule wakala.
 

Ukisikia mtu anajieleza kwa nguvu tuna ofisi japan na bongo au china na Tanzania kaa kijanja
 
Background ya Umaskini na tamaa ya kutaka mafanikio ya haraka ndio sababu kuu zinazopelekea wafanyabishara wa bongo kuwa jinsi walivyo.
 
Hivi huyu jamaa ameweza kuku-twist mpaka ukalainika? Unaona kweli hiyo link aliyoweka ni forum yenye hadhi ya kuaminika? Angalia usije kulizwa hapa. Tumieni website zinazoaminika ambazo umepewa link, hizo za Befoward na hiyo nyingine.
Kaka,
Jamaa hajanitwist niliona ameweka web yake nami nikapitia ni kama middle man. Uzi wangu haujasema wote ni matapeli ila nimetoa tahadhari maana watu wengi wanalizwa mno.
Mimi nishakutana nao sana na siwezi kuagizia gari kupitia middle man kabsa na sishauri mtu aagize gari kupitia hawa watu....

Though kuna wengine ni waaminifu ila ni nadra sana....
 
Asante kwa kutoa ushuhuda kaka.

Kwa kuongezea ukiona gari kwa hawa jamaa jaribu hata kusearch ile picha kwenye google utaona maajabu....
 
Mkuu acha tu
 
Watanzania matatizo sana.

Watu wanapigwa sana. Yaani kama kariakoo watu wanatumia simu miezi 8, wanaisafisha kisha wanaifunga kwenye boksi.

Yaani mtu ananunua simu unakuta kuna namba au sms ya mtu imesahaulika kufutwa.

Huu ujanja ujanja ndio unafanya biashara zetu ziwe duni. Tamaa na utapeli mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…