Jihadhari na matapeli hawa wa Kupatana.com

Mkuu nikuulize kwani hizo amazon au ebay ziliamka tuu zikawa world wide?
Nakutakia asubuhi njema.

Kwenda world wide ni mipango ya kampuni na kupatana haiwezi kwasababu haina uwezo wa kumlinda mteja wake kama hizo kampuni nyingine.
Mtu kaandika yuko Dar,unamtext anasema yuko Kenya,unamuliza jina la duka lake anakutajia jina feki halafu unataka kufanya nae biashara wakati kuna kashaonyesha utapeli mpaka hapo?
Ebay,Amazon huwezi kutana na vitu kama hivyo.
 
hata mimi, sijui wamepata wapi namba na kujua nna kijana anasubiri kwenda JKT
 
Kuna siku nliingia kupatana nkakuta kuna mtu anauza laptop flan nkaipenda. So nkachukua namba yake na kwa kua alisema yupo DSM nikampigia. Baada ya maongez akaniambia yeye yupo Iringa maeneo ya kihesa, bahat nzuri hapo kihesa nina mdogo wangu anaish huko nikamconnect nae akaone mzigo then ikiwa fine mimi nitume pesa kwa dogo achukue mzigo. Dogo baada ya kumpigia jamaa akabadili tena location akasema yupo Tunduma. Ilibidi nicheke kwa kujua matapel wako kwenye harakat zao. So far mim na kupatana tumeshatalakiana.
 
Bado tunakuja palepale. Ndo maana wabongo wengi hatuendelei kwa sababu tunalimit possibilities. Hawawezi kumlinda mteja sawa sikatai, je umeambiwa hawatoweza?
Naaamina hata kama kuna memba wakongwe humu watatupa ushuhuda jamii forum ilivoanza ilivokua na sasaivi ikoje.
 
M sitosahau jamaa la iringa lilikulaga laki mbili zangu kizembe nilidanganywa na uustadhi wake nikamuamini kumbe ndo najitumbukiza shimoni
Huyo ustadhi unakuta ni kaka ake au ni yeye mwenyewe anakupigia sim [emoji21] pole mkuu. Najua laki mbili zinauma hasa kipindi hiki cha tingatinga
 
Naona unajichanganya tu.
 
In short huyu wa iringa hafai kuitwa tapeli. Huyu ni Mwizi kabisaa maana hana hata technique.
 
Huyo ustadhi unakuta ni kaka ake au ni yeye mwenyewe anakupigia sim [emoji21] pole mkuu. Najua laki mbili zinauma hasa kipindi hiki cha tingatinga
Nilijionaga mjinga Mara mbili make isingekuwa tamaa nisingeliwa afu kupenda vitu cheap na kingine kimwamini mtu nisiyemjua kisa anajua vifungu vya quran
 
Nilijionaga mjinga Mara mbili make isingekuwa tamaa nisingeliwa afu kupenda vitu cheap na kingine kimwamini mtu nisiyemjua kisa anajua vifungu vya quran
Yaani mkuu watu wengi wanakunjuaga wakishatajiwa au kuambiwa kua "MIMI NI MTU WA MUNGU" yaani hapo ndo unakuta maskini mtu unamuamini alafu ndo anakupiga pigo moja mithili ya judo
 
Yaani mkuu watu wengi wanakunjuaga wakishatajiwa au kuambiwa kua "MIMI NI MTU WA MUNGU" yaani hapo ndo unakuta maskini mtu unamuamini alafu ndo anakupiga pigo moja mithili ya judo
Ndo hivyo nilikuwaga sijawai tapeliwa ila tangu siku ile akili ilinikaa sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…