Pianist
JF-Expert Member
- Nov 7, 2010
- 681
- 372
Kuna matapeli wanapita mitaani na gari na kujifanya wao wametumwa na TRA kuangalia biashara ndogondogo kama saluni, stationery, magenge na maduka kama zimesajiliwa. Hawana vitambulisho na gari wanayotumia ina namba za usajili za kiraia. Wakikuta hauna leseni na TIN number wanatoa vitisho vya faini kubwa (laki tano, milioni) na kisha kuomba rushwa (elfu hamsini) na kuchukua baadhi ya bidhaa unazouza kama; kopo la maziwa ya unga, dumu la mafuta ya kula bila ya kuwa na aibu. Hawa ni wezi na matapeli kama walivyo wengine. Siku ukiwaona wapo kwenye sehemu ya biashara ya mtu mjulishe mhusika kwamba hao ni wezi asiwape rushwa.