Jihadharini na utapeli wa mauzo kwenye maduka

Jihadharini na utapeli wa mauzo kwenye maduka

jigili

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
350
Reaction score
344
Tarehe 7/12/2024 kuna mteja alifika kwenye duka linalouza vifaa vya umeme kununua mojawapo ya bidhaa za umeme bahati mbaya akawa amekuja na kiasi cha pesa pungufu akaomba muuzaji aongee na bosi wake ambaye hakuwepo wakati huo amkubalie kununua kwa bei hiyo.

Baada ya muuzaji kumaliza kuongea na bosi wake na bosi kukataa kuuza kwa bei hiyo, mteja aliomba simu ya muuzaji ili arudishe mrejesho kwa aliyemtuma, kitendo cha muuzaji kumpa simu likawa kosa akatazama muuzaji kasave jina la bosi wake namna gani na yeye akasave namba yake kwenye simu hiyo kwa jina hilo hilo.

Baada ya hapo akarudisha simu akaondoka zake, baada ya muda kidogo muuzaji akapokea ujumbe kwenye simu yake wenye jina la bosi wake anamuelekeza atume mauzo ya leo kwenye namba fulani bahati nzuri muuzaji alijiongeza kwa kujaribu kumpigia ili ampe ufafanuzi zaidi sababu haikuwa utaratibu wao wa kila siku, hapo ndipo aliposhtuka namba iliyotumika si ya bosi wake bosi hakuwa na taarifa yoyote kuhusu ujumbe huo.
 
Back
Top Bottom