Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Napenda kuwatahadharisha wadau wote kuwa muwe makini zaidi mkiwa barabarani hasa kwenye foleni jijini Dar kwani kuna kundi la vijana zaidi ya 30 maarufu kama 'KIBOKO MSHELI' wanaovamia magari wakiwa na mapanga,nondo na visu kwa lengo la kupora chochote ulichonacho na halikadhalika wanaua ama kujeruhi.
Maeneo hatari ni maeneo ya Jangwani- Morogoro Road,Ocean Road, Seaview, Salender Bridge, Bonde la Kigogo ukitokea Ilala kuja Magomeni, Daraja la Ubungo karibu na njia panda ya kwenda UDSM na barabara ya Mandela Road ukitokea Tazara kuja Ubungo (NDIPO ALIPOVAMIWA RAFIKI YANGU)
His Case.
Akiwa kwenye folen majira ya saa mbili usiku, ghafla lilitokea kundi la vijana kama kumi na mapanga na kuanza kupiga vioo vya gariwakitaka kuvunja, aidha waliongezeka ghafla na wakafunga barabara kama kwa dk 7 hivi wakiendelea kumshambulia (kwenye gari walikuwa watatu),kumbuka kwenye foleni huwezi kukimbia popote, Mungu aliwasaidia sana kwani milango ya gari ilikuwa imefungwa/locked, na vioo vilikuwa vimefungwa kasoro kimoja kilikuwa wazi nusu.
Baada ya mapambano na kelele za kuomba msaada,ndipo msamalia mwema aliyekuwa na silaha aliingilia kati na ndipo alipowatawanya.Kwa mujibu wa Taarifa mbalimbali, haya matukio yamekuwa yakiongezeka sana katika siku za usoni, kwa hilo nawatahadharisha msinunue vitu ovyokwenye traffic light, vioo msishushe ovyo na lock za milango ya magari mfunge, muwe makini.
Ujambazi huu unafanyika kila siku sehemu tofauti kuanzia saa 12 jioni kuendelea.
Namshukuru Mungu hakuna aliyeumizwa sana, japo walifanikiwa kupata baadhi ya vitu ikiwemo simu ya mwenye gari.Natambua unaweza kuona kama sinema,ila haya ndio yanayotokea katika jiji la Dar kwenye foleni za magari.