JIiwe hili Jiwe gani, hapa kwetu kijijini ?

kitunguu saumu

New Member
Joined
Apr 23, 2020
Posts
4
Reaction score
8
JJIWE HILI JIWE GANI HAPA KWETU KIJIJINI?

Kwenye mwanga waliona, kwenye giza hulioni,
Waliokwisha liliona, wakatoa zao warn,
Wa kijiji wakagoma, wakaziba zao mboni,
Jiwe hili Jiwe gani, hapa kwetu kijijini?

Wale waliolileta, nao sasa wanajuta,
Linawapiga mieleka, na viuno kuvunjika,
Wasotaka fedheheka, wanalipaka mafuta,

Waandishi wa habari, wajua madhara yake,
Kulipamba ni hiari, na picha zake uweke,
Kutofanya ni kiburi, akili kando uweke,

Tukatoboa na tundu, ila nalo likazibwa,
Gwanda, bendera,vifungu, saa nane vikaibwa,
Pakajawa na ukungu, kuliona kawa shida

Upande wa mashariki, linapo tokea jua,
Hua hauathiriki,hata inyeshe mvua,
Eti hakuna riziki, mbolea imekwangua,

Wakazi kwenye kijiji, nao wamegawanyika,
Wasemao hawashibi,jiwe shamba lafunika,
Na wenginewaahidi, nguo zao waanika

Lilipachokwa kwa chuma, halikupaswa liwepo,
Wengi walolisukuma, wana enjoy upepo,
Waloachaga huruma, upande wao si heko.

Jiwe hili ni kimondo, jiwe hili ni dhahabu?
Jiwe hili lina mambo, jiwe hili kama dubu,
Lapaswa liwekwe kando, watu wasilihusudu,

Ona najihatarisha,nataja mambo ya jiwe,
Hili jiwe linatisha, hupenda sifa lipewe,
Mabayake nakanusha, kwa jiwe vigelegele
Ali li li li li li li li li li li li li li li li li li
Jiwe jiwe jiwe jiwe jiwe jiwe jiwe jiwe.
 
Sawa nakubali wewe ni hodari kwenye utunzi ila kuwa makini aisee,jiwe halipendi ukweli.
 
Karibu sana jf
Screenshot_20200423-225253.jpg
 
Kile ukitafutacho, hakika utakipata,
Kikombe achana nacho, mwana haramu apita,
Twakusihi uwe macho, hatupo kukutafuta,
Mkuu 'si twakupenda, sikiliza ushauri.
 
M
JJIWE HILI JIWE GANI HAPA KWETU KIJIJINI?

Kwenye mwanga waliona, kwenye giza hulioni,
Waliokwisha liliona, wakatoa zao warn,
Wa kijiji wakagoma, wakaziba zao mboni,
Jiwe hili Jiwe gani, hapa kwetu kijijini?

Wale waliolileta, nao sasa wanajuta,
Linawapiga mieleka, na viuno kuvunjika,
Wasotaka fedheheka, wanalipaka mafuta,
Jiwe hili Jiwe gani, hapa kwetu kijijini?

Waandishi wa habari, wajua madhara yake,
Kulipamba ni hiari, na picha zake uweke,
Kutofanya ni kiburi, akili kando uweke,
Jiwe hili Jiwe gani, hapa kwetu kijijini?

Tukatoboa na tundu, ila nalo likazibwa,
Gwanda, bendera,vifungu, saa nane vikaibwa,
Pakajawa na ukungu, kuliona kawa shida
Jiwe hili Jiwe gani, hapa kwetu kijijini?

Upande wa mashariki, linapo tokea jua,
Hua hauathiriki,hata inyeshe mvua,
Eti hakuna riziki, mbolea imekwangua,
Jiwe hili Jiwe gani, hapa kwetu kijijini?

Wakazi kwenye kijiji, nao wamegawanyika,
Wasemao hawashibi,jiwe shamba lafunika,
Na wenginewaahidi, nguo zao waanika
Jiwe hili Jiwe gani, hapa kwetu kijijini?

Lilipachokwa kwa chuma, halikupaswa liwepo,
Wengi walolisukuma, wana enjoy upepo,
Waloachaga huruma, upande wao si heko.
Jiwe hili Jiwe gani, hapa kwetu kijijini?

Jiwe hili ni kimondo, jiwe hili ni dhahabu?
Jiwe hili lina mambo, jiwe hili kama dubu,
Lapaswa liwekwe kando, watu wasilihusudu,
Jiwe hili Jiwe gani, hapa kwetu kijijini?

Ona najihatarisha,nataja mambo ya jiwe,
Hili jiwe linatisha, hupenda sifa lipewe,
Mabayake nakanusha, kwa jiwe vigelegele
Ali li li li li li li li li li li li li li li li li li
Jiwe jiwe jiwe jiwe jiwe jiwe jiwe jiwe.
Mmmh
 
Back
Top Bottom