Jiji la Dar es Salaam linanuka harufu za ajabu ajabu

Jiji la Dar es Salaam linanuka harufu za ajabu ajabu

koba lee

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2016
Posts
981
Reaction score
1,606
Kwema wakuu?

Twende kwenye mada husika. Narudia jiji hili linanuka harufu ya miozo kwa sehemu nyingi. Mtu mbwa wake kadanja anamchukua anamtupa barabarani au pembezoni mwa barabara, paka, mbuzi, kuku wote vilevile.

wanatupwa sehemu ambazo ni makazi ya watu au pembezoni mwa barabara. Hii inasababisha harufu karibia mtaa mzima, iwe una kaa maeneo hayo au ni mpita njia basi ni miharufu mwanzo mwisho. Yaani ni kama mtu kashikilia switch ya kuruhusu harufu itoke au ikate, mfano umepanda gari tokea temeke unaelekea G/Mboto.

Ukifika Sokota ni harufu ya uozo, sokoni na Tazara ni utulivu, Vingunguti ni uozo, Kipawa amani tele, majumba sita uozo mwanzo mwisho, yaani unafika mwisho wa safari kichwa kinauma. Nadhani wengi wenu ni mashuhuda wa hali hii hasa wakazi wa Dar iwe una usafiri binafsi au wa jumuiya.

Hali ni tete Mtu kwa akili zako timamu huwezi tupa mzoga wa mnyama kiholelaholela tu kuna taratibu zake, na hiki kinaweza kua chanzo cha magonjwa mapya ambayo hayaeleweki. Nadhani kuna sheria ndogondogo inabidi ziundwe kudhibiti hii hali tena mabwana /bibi afya walivalie njuga hili suala.

ikitokea mwenyekiti wa mtaa, mtaa wako una harufu ya uozo basi awajibishwe kwa mujibu wa sheria. Unakuta mtu ana kibanda chake cha chips lakini katika eneo hilohilo kuna miharufu ya uozo tena yeye habari hana, huyo achukuliwe.

Nyingine kwenye daladala au mwendokasi asubuhi tu watu mnaenda kazini, unakuta mtu ananuka kama ng'onda, harufu ya kwapa, jasho ,mdomo yaani balaa. Asubuhi tu hiyo sijui jioni itakuaje.

Anyways ngoja niishie hapa lakini nadhani ujumbe umefika japo mi sio muandishi mzuri.

Wasalaam.
 
Jiji linatakiwa liwe Safi kwa kulisafisha kila wakati haijalishi nani katupa nini

Tunajua watu ni wachafu na hawajali hata kama mtaro utaziba au la lakini ni wajibu wa wahusika kuwapiga faini hao na Halmashauri ya jiji waweke efforts zaidi badala ya kuiba hela za usafi

Jiji linanuka kwa sababu hakuna uangalizi ni kama nyumbani kwako tu
Hela zinatoka za bajeti zinaenda wapi?
Watu wanalipa kodi, Tozo kila kona mpaka za usafi tunalipa wakati sio kazi yetu
 
Jiji linatakiwa liwe Safi kwa kulisafisha kila wakati haijalishi nani katupa nini

Tunajua watu ni wachafu na hawajali hata kama mtaro utaziba au la lakini ni wajibu wa wahusika kuwapiga faini hao na Halmashauri ya jiji waweke efforts zaidi badala ya kuiba hela za usafi....
Nunga mkono hoja mkuu. Nakumbuka enzi za uongozi wa makonda kulikua na utaratibu kua kila Jmosi ni usafi mpaka saa 4 asubuhi. Hakuna kufungua biashara yoyote ndani ya muda huo, na kweli jiji kidogo lilipendeza. Lakini hivi sasa ni kama jalala.
 
uchafu, mipangilio mibovu ya makazi, biashara nk.. Barabara zimechimbwa kila mahala yaani kila siku ujenzi.

Tunahitaji kubadirika pakubwa sana na wahusika waanze kuweka akili kwenye maendeleo ya nchi na sio maendeleo binafsi.
 
Back
Top Bottom