Revolution
JF-Expert Member
- Feb 28, 2008
- 960
- 927
Dodoma ni Jiji linalokuwa kwa kasi sana na ni Mji wa Kiserikali kama ilivyo kwa Lagos, Nigeria na Pretoria, Afrika Kusini.
Kero mojawapo kubwa ambayo inakera kweli kweli ni kutopatikana kwa maji ya uhakika. Maji Dodoma kwa baadhi ya maeneo ni nadra sana kupatikana.
Rai yangu ni kuwa Serikali chini ya Kiongozi wetu mpendwa na mpenda maendeleo Mh. Dkt Samia, itatue hii kero mara moja na kwa haraka ili kulifanya Jiji hili kuwa ni mji wa kisasa wa Serikali wenye hadhi kama majiji mengine.
Serikali inashindwa nini kuvuta maji kutoka Mtera? Au Mto Wami na kuyaleta hapa kuliko kutegemea maji ya visima?
Population inaongezeka kwa kasi lakini upatikanaji na usambazaji wa maji haundani na ongezeko la watu. Mfano eneo la AREA D ambapo kuna viongozi wengi kuna shida ya maji sana, swaswa, Meliwa na Kisasa ni tabu kweli kweli.
Ni ipi kero nyingine unayokumbana nayo hapa Dodoma?