Jiji la Mbeya lingeiuza club ya Mbeya City

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Hii timu ilianza vizuri na ilikuwa mashabiki wengi sana. Lakini miaka ya karibuni inakufa kidogokidogo na msimu huu sidhani kama itaweza kubaki ligi kuu. Ni wazi kuwa wamiliki wake wameshindwa kabisa kuiendesha na nafikiri halmashauri kupunguziwa sehemu ya mapato kumechangia.

Naona kuwa uamuzi wa busara ni kuiuza hii timu walau mpate chochote vinginevyo inaenda kuwafia kabisa. Uzeni na pesa fanyieni jambo la maana kama shule au kujenga uwanja wa michezo.
 
Watamuuzia nani sasa! Hapo ndipo shughuli ilipo.
 
Yani timu hiyo hiyo wauze wapate hela ya kutosha kujenga uwanja? Kuwa serious bro, Kwa Mbeya city hii labda wauze kisha wapate hela za kununulia noah used
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…