Jiji la Mwanza: Tunataka huduma ya mwendo kasi (Mwanza Rapid Transport)

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,446
Reaction score
1,645
Habari Tanzania !

Nawaomba sana maana kumekuwa na changamoto kubwa sana ya Usafiri wa Umma Mkoa wa Mwanza.

Mwanza ya sasa sio ile ya zamani; maana kuna idadi kubwa sana ya watu na watu wanateseka kwa usafiri maana mwendo kasi vyombo vya usafiri ni mdogo na vyombo vingi ni chakavu sana.

Wenye mamlaka na wadau wa Usafiri fanyeni basi kitu hapa Mwanza.

Karibu.
 
Ombeni kwanza mpate watu wenye weledi kuweza kusimamia huo mradi vinginevyo mtateseka kama wa Kimara na Mbezi
 
Ombeni kwanza mpate watu wenye weledi kuweza kusimamia huo mradi vinginevyo mtateseka kama wa Kimara na Mbezi
Tumeanza na maombi hapa kwanza Jamii Forum; maana walishawahi kukiri kuwa hapa jukwaani huwa wanapitapita mara moja moja.

Watusaidie sisi Mwanza maana tumekuwa wahanga wa Usafiri; tupate raha ya usafiri jamani.
 
kama madraja mawili (Mkuyuni na Mabatini) tu yana miaka karibia miwili hayajakamilika, hiyo mwendo kasi mtaiweza
Kiufupi Mwanza hata sasa barabara za kwenda mjini kati na kutoka ni kero, sikuamini nilichokiona last week
Jiji pekee duniani ambalo kidaraja cha kawaida kinajengwa kwa two years
 
Tutawaletea parachute maana mnaishi milimani
Watuletee Mwanza Van Wire Electricity Transport. Mfano, moja inafungwa pale Nyakurunduma (Mkuyuni) kwenda Bugando Hospitali. Hii itakuwa unyama sana maana ni mwendo wa ngiri.
 
Mtasumbuka tu hakuna kitu itawasaidia, huku bongo tangu Mkulungwa wetu baba la baba aende mbinguni tumekuwa tukijazana vituoni tu kama ng'ombe mnadani, cha kuwashauri labda muwaombe wawekezaji waongeze magari mjini na serikali itanue njia labda mtapona.
 
Hmm huku nyamagana barabara tu zimewashindwa kurekebisha ukienda machinjioni-kakebe kama uko sijui mkoa gani! Labda…
 
Mambo ya kishenzi kabisa, tuendelee kuvumilia🥲
 
Daraja la mabatini hilo ni kituko.Two years😂
 
Madaraja ujenzi umeisha ama unatafuta kujipendekeza tu!!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…