Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Mvua hiyo iliyoanza saa 12 asubuhi pia imesababisha msongamano mkubwa wa magari huku watu wakilazimika kupita juu ya maji.
Maji yameshuhudiwa yakielekea katika ya barabara nyingi za katikati ya jiji hilo kubwa la Afrika Mashariki, mafuriko ambayo wakazi wanasema hayajawahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.
Barabara zilizoathiriwa na mafuriko hayo ni pamoja na Moi Avenue, Tom Mboya, Racecourse, Ronald Ngala, Haile Selassie Avenue, Temple Road na barabara ya Kimathi.
Barabara kuu ya kwenda mji wa pili kwa ukubwa Mombasa pia imeathiriwa na mvua hiyo na kujaa maji.
Mvua kubwa imekuwa ikinyesha nchini Kenya katika siku za hivi karibuni huku mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo ikionya kuwa mvua kubwa itaendelea kushuhudiwa katika siku zijazo.
Wito umetolewa kwa watu katika maeneo ambayo kuna mafuriko, kwenda katika maeneo yaliyoinuka, kuepuka maafa zaidi.