Uchafu uliokithiri jijini,
Msongamano wa magari unaokera,
Ongezeko la Ombaomba Barabarani,
Kuongezeka kwa watu wanaofanya biashara kwenye maeneo mbalimbali kiholela mfano Manzese, na sehemu kadhaa za barabarani
Pamoja na mengine mengi....Ni ishara kuwa Jiji hili limemshinda Mheshimiwa huyu ambaye pia ni mbunge wa Isimani?
Ha ha ha ha. Ni mmoja wa wale waliotajwa katika kile kitabu cha mafisadi wa elimu!! Ngoja ni break kidogo nirudi ninukuu wasifu wake toka ndani ya kile kitabu nitumbukize hapa!!
Hatujaridhika mkuu na Ndio maana tumeanza kwa kupaza sauti zetu kupitia JAMII FORUM na hii ni kuonyesha kuwa tumechoka.Naamini wahusika wameshasikia haya yote lakini wakiweka pamba masikioni wajue kila kitu kina mwanzo na mwish.Ipo siku ambayo Hatua za juu kutoka kwa wananchi zitachukuliwa.ila kama wananchi wa Dar es salaam tupo "comfortable/relaxed" /tunafurahia hali hii, hakuwezi tokea miujiza.
historia inaonyesha changes nyingi zinatokana na wananchi kutoridhishwa na mifumo mibovu na ya kinyonyaji na hivyo kuonyesha kwa vitendo kutoridhishwa huko. iwe kwa maandamano, migomo au namna yoyote ile.
inaonekana hapa Dar everybody is happy, watu wanalalamika chinichini tu oooh mara Lukuvi, oooh mara diwani, ooooh mara meya nk. siku zinakwenda na watu wanajinafasi na wananawili na wanazidi kujijenga. mwisho wa siku wanakuwa hawakamatiki kwani wameshaiba vya kutosha
Tatizo sio Lukuvi ila ni miundo mbinu ya siku nyingi toka wakati ule wa ukoloni mpaka leo bado yanafanya yale yale pamoja na kuongezeka kwa watu katika dar lakini hakuna barabara za kutosha na vitu kama hivyo, sio Lukuvi ni utaratibu mbaya wa serikali na mambo yake
Hatujaridhika mkuu na Ndio maana tumeanza kwa kupaza sauti zetu kupitia JAMII FORUM na hii ni kuonyesha kuwa tumechoka.Naamini wahusika wameshasikia haya yote lakini wakiweka pamba masikioni wajue kila kitu kina mwanzo na mwish.Ipo siku ambayo Hatua za juu kutoka kwa wananchi zitachukuliwa.
Kuleta ya kwene kitabu ni kutafuta majawabu rahisi kwa maswali magumu. Hakuna uhusiano.
Kumbe ni kamradi kamebuniwa ka kuinuana wakati jiji linazidi kudidimia kila siku.Shame on us!
Uchafu uliokithiri jijini,
Msongamano wa magari unaokera,
Ongezeko la Ombaomba Barabarani,
Kuongezeka kwa watu wanaofanya biashara kwenye maeneo mbalimbali kiholela mfano Manzese, na sehemu kadhaa za barabarani
Pamoja na mengine mengi....Ni ishara kuwa Jiji hili limemshinda Mheshimiwa huyu ambaye pia ni mbunge wa Isimani?
Tatizo wananchi wenyewe wa jiji la Dar ni wachafu Lukuvi ataweza wapi?? huko mitaani kwenu,,mnamwaga takataka barabarani halafu mnamlaumu Lukuvi unataka yeye aje akuonyeshe jinsi ya kutunza taka?? Jipangeni wenyewe kwenye mitaa yenu halafu ndipo muone kama kutakua na uchafu....angalieni moshi kule ukitema mate tu ovyo jirani yako anakushitaki serikali za mitaaa
Hivi tunavyobwabwaja humu ndani tunajua vizuri job description ya RC?Lukuvi asilaumiwe kwa matatizo ya jiji ,mfumo wa sasa wa manispaa tatu kila moja na utawala wake kamili na jiji na ofisi ya mkuu wa mkoa inakuwa kama kambare hakuna mdogo wote wana masharubu na kila manispaa inapanga mambo yake ni vizuri jiji likaundwa upya kwa kuweka mfumo mzuri na kulifanya kuwa madaraka na mapato ya kutosha kutokana na vianzia vilivyopo katika jiji mfano bandari ili liweze kutoa huduma muhimu kwa jiji lote na kuboresha miundombinu na mamlaka zinazotoa huduma kama dawasa, tanesco na tanroad mkoa wa dar .ni vizuri ziwe coordinated na jiji na mtendaji wake mkuu apewe meno ya kutosha na kuwe na masterplan itakayo ongoza ukuaji wa dar kwani kwa sasa iliyopo imeshakwisha muda wake.
Mimi naona sisi hatujui hata kidogo kazi za RC na majukumu yake katika jamiiHivi tunavyobwabwaja humu ndani tunajua vizuri job description ya RC?
Josh hebu tujuze vyema kazi na majukumu ya RC.Mimi naona sisi hatujui hata kidogo kazi za RC na majukumu yake katika jamii
Mi naona unamuonea Lukuvi bure. Labda utuambie ni nani aliyelimudu. Makamba? Ditopile?Kandoro?Chipungahelo?............
Mi naona hakuna mwenye afadhali! Wote wamelishindwa kama huyu bwana mkubwa Lukuvi.
Uchafu uliokithiri jijini,
Msongamano wa magari unaokera,
Ongezeko la Ombaomba Barabarani,
Kuongezeka kwa watu wanaofanya biashara kwenye maeneo mbalimbali kiholela mfano Manzese, na sehemu kadhaa za barabarani
Pamoja na mengine mengi....Ni ishara kuwa Jiji hili limemshinda Mheshimiwa huyu ambaye pia ni mbunge wa Isimani?