Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Epuka moshi kutoka kwenye moto wa kupika kwasababu una vitu vidogo ndani yake ambayo vinaweza kuingia kwenye mapafu na kusababisha ugonjwa
Epuka moshi huo kwa kupikia nje au mahali penye hewa safi ambayo moshi unaweza kuingia na kutoka
Kuna aina ya viini vinavyoitwa bakteria na vingine vinavyoitwa virusi. Virusi husababisha kikohozi na mafua na vinaweza kuuawa kwa kutumia dawa.
Hivyo ukiathiriwa na bakteria au virusi katika mfumo wako wa upumuaji tafadhali nenda kamuone Daktari
Komesha kikohozi, mafua na magonjwa mengine kutoenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
Ili kufanikisha hilo hakikisha mikono na vyombo vya chakula na maji ni safi, tumia karatasi maalum au kitambaa safi wakati unakohoa