Asante, Mkuu kwa uhamasishaji huu wa kuvaa barakoa.
Hata hivyo, zipo shuhuda za watu mbalimbali ambao wametumia barakoa kwa muda mrefu hasa kwa safari ndefu kuhishiwa nguvu!! Imewatokea baadhi ya watu ninao wafahamu! Salama yao ilikuwa kuzivua na kuvuta mpumzi nyingi kuiingiza kifuani na kisha kuitoa taratibu kwa karibu mara kumi! Hii ni kwa mtu anayeelewa chanzo cha kuishiwa nguvu zake! Kwa asiye elewa inaweza kuwa balaa.
Kwa hiyo, mbali na nia njema hiyo kujaribu kudhibiti korona kwa barakoa, wahamasishaji wa matumizi ya mabarakoa wanatakiwa kutoa na maelekezo ya madhara ya uvaaji barakoa na namna ya kuyakabili.