Samedi Amba LLC
Member
- Apr 5, 2024
- 81
- 117
Habari wanaJF,
Natuamini kuwa mnaendelea vizuri. Mungu amekuwa mwema sana sana kwangu. Nimepotea siku 2, 3 hizi (nlikuwa nahudumia jamii na kumalizia msiba wa ndugu mmoja hivi). Sasa nimerudi kuendelea na makala yetu ya kujikomboa kiuchumi.
Nimejificha kwenye maktaba fulani hapa. Feni zinafanya kazi yao (Morogoro ina kajoto sasa hivi). Yote mema!
Katika masomo mawili yaliyopita, tulizungumzia hatua 2/7 ya kujikomboa kiuchumi:
Majanga yetu ya Tanzania ni pamoja na:
❌ Kupoteza kazi – Kibarua kinaweza kuota nyasi muda wowote.
❌ Matibabu ya ghafla – Si kila mtu ana bima ya afya, na gharama za hospitali zinaweza kuwa mzigo mkubwa.
❌ Majukumu ya kifamilia – Kuna mtu huko nje anaweza kupatwa na shida. Unaweza kumpoteza mzazi au ndugu wa karibu ukalazimika kusafiri mwendo mrefu na kutoa matumizi msibani.
❌ Kudorora kwa biashara – Ikiwa una biashara, unaweza kukabiliana na mauzo duni, wateja kuchelewa kulipa mikopo, na mabadiliko yasiyotegemewa.
❌ Mabadiliko ya kiuchumi au kisiasa – Mabadiliko ya bei, kushuka kwa thamani ya fedha, au sera mpya za serikali zinaweza kuathiri mapato yako. (Kawaida, vitu hivi huwa nje ya uwezo wako).
Unapaswa Kuweka Akiba Kiasi Gani?
Awali ya yote, kaa chini na kutambua matumizi yako ya mwezi kwa vitu muhimu: kodi ya nyumba, chakula, umeme, maji, nauli, mafuta (kama una chombo cha moto), mavazi nk. Piga hesabu, halafu tanua wigo kidogo. Kwa mfano, kama matumizi yote ni 189,500, unaweza kukadiria 200,000. (Laki 2 ndo itakuwa matumizi ya mwezi mmoja).
Baada ya kutambua hilo, fanya hivi:
1️⃣ Anza na kiashi kidogo– Hifadhi angalau mwezi mmoja wa matumizi (kwa mfano wa leo, laki 2).
2️⃣ Wafanyakazi – Weka akiba ya miezi 3–6 ya matumizi yako yote (kwa mfano wa leo, itakuwa laki 6 hadi 1.2m).
3️⃣ Wafanyabiashara/wenye ajira binafsi– Hifadhi kiasi sawia na angalau miezi 6 hadi 12 ya matumizi, kwani siku hazilingani. Kiasi kinakuwa kikubwa kwa sababu unashughulikia matumizi ya nyumbani na ya biashara pia.
Kwa wanafamilia: Unaweza kulenga TZS 6M au zaidi. Maisha na majukumu hayasubiri, na mawimbi yake hayajulikani.
Hela Hizi Uzitunze Wapi?
Akiba yako ya dharura inapaswa kuwa:
✅ Rahisi kufikiwa – Lakini isiwe rahisi kiasi cha kutumiwa hovyo.
✅ Salama dhidi ya mawimbi ya kiuchumi– Epuka kutunza fedha sehemu ambapo hamna usalama. (Ntakupa mbadala hivi karibuni. Tutakuja kuzungumzia UTT-AMIS, bond za serikali, na Money Market Funds (MMF) baadaye).
Unaweza kutumia:
🔹 Akaunti za simu (M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas) – Zingatia gharama za kutoa. MPESA wana products kama MGODI, MPAWA nk ambazo zinaweza kukupa riba kidogo kwa mwezi/mwana.
🔹 Akaunti za akiba benki – Chagua benki isiyo na makato makubwa. CRDB na NMB wako vizuri (ongea na afisa uwekezaji kwanza kujiridhisha).
🔹 SACCOs/Vikoba vinavyoruhusu utoaji pesa haraka
🔹 Akaunti za muda maalum (fixed deposit, miezi 3–6) – Itakusaidia unapokuwa na lengo fulani la mbeleni.
🔹 Akiba ya pesa taslimu (endapo hakuna benki karibu) – hakikisha fedha zimehifadhiwa vizuri, na uwe macho endapo noti zitabadilishwa.
🔹 Akiba ya katika madini maalum – Dhahabu ni nzuri sana katika hili. Thamani yake huwa haishuki ovyo, na haiozi (doesn't expire). Unaweza kununua kipande cha dhahabu, ukaikatia risiti, kisha ukatunza kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
Endapo kipato chako ni kidogo, fanya hivi:
💰 Tumia kanuni ya 5hadi25 – Weka 5% hadi 25% ya pesa yoyote unayopata kulingana na kipato chako.
💰 Punguza matumizi yasiyo ya lazima – Epuka anasa kama kula vitu usivyohitaji, kuishi bila bajeti au kuchukua mikopo ya simu bila sababu.
💰 Uza vitu visivyotumika – Simu za zamani, fanicha, au vitu vingine vya nyumbani vinaweza kuleta pesa za ziada.
💰 Tafuta kazi ya ziada– Fikiria kazi ndogo yoyote inayoweza kukuongezea kipato.
Akiba ya dharura itakupa:
✅ Kinga unapopoteza kazi – Jua pa kuanza kazi inapoisha.
✅ Kijitegemea bila mikopo – Hutalazimika kukopa kwa dharura kutoka kwa marafiki.
✅ Amani ya akili na moyo – Utaanza kuwazia maendeleo, sio kuhangaikia changamoto za kifedha.
✅ Nguvu ya kuhudumia familia na jamii yako – Kusaidiana ni desturi yetu Tanzania. Kuwa na fedha ya kutosha inakupa shavu ya kuchangia misiba, kuwasapoti wazazi wako, na dharura zingine katika jamii (na heshima juu). Hutasumbukia ada ya shule (aka kuongea na mwalimu January), chakula, na matumizi ya mke wako (kama unaye).
Hitimisho
Hatua hii inaweza kuchukua muda, lakini ni ya thamani. Akiba ya dharura inakupa uhuru, usalama, na udhibiti wa maisha yako ya kifedha. Anza leo, hata kama ni kwa TZS 1,000 tu kwa wakati mmoja!
Natuamini kuwa mnaendelea vizuri. Mungu amekuwa mwema sana sana kwangu. Nimepotea siku 2, 3 hizi (nlikuwa nahudumia jamii na kumalizia msiba wa ndugu mmoja hivi). Sasa nimerudi kuendelea na makala yetu ya kujikomboa kiuchumi.
Nimejificha kwenye maktaba fulani hapa. Feni zinafanya kazi yao (Morogoro ina kajoto sasa hivi). Yote mema!
Katika masomo mawili yaliyopita, tulizungumzia hatua 2/7 ya kujikomboa kiuchumi:
- Jiwekee akiba ya mwanzo (starter emergency fund), kwa ajili ya kutatua matatizo madogo madogo. Utaacha kupiga simu za "nipige tafu". Tulishauri 100,000 kwa wenye kipato cha chini (mlinzi, garden boy na mdada wa kazi), mshahara wa mwezi 1 (kwa wafanyakazi), na 1m-3m+ kwa wafanyabiashara. Uzi huu hapa.
- Lipa madeni yako yote, ili kuondokana na uwekezaji wa kurudi nyuma. Madeni hukwamisha mambo mengi, na hasa ukichukua deni kwa ajili ya chakula na matumizi ya kawaida. Uzi huu hapa.
Umuhimu wa Kuwa na Kinga ya Kiuchumi
Mpaka unafikia hatua hii ya tatu, utakuwa umesuluhisha tatizo kubwa linalowakumba watu wengi hapa Tanzania. Watu kama Jay Jay Okocha, Ronaldinho Gaucho, na Mike Tyson wanatukumbusha kuwa hitaji kubwa la wanadamu sio mihela mingi, bali nidhamu katika kila hatua. Usiwe kama wao.Majanga yetu ya Tanzania ni pamoja na:
❌ Kupoteza kazi – Kibarua kinaweza kuota nyasi muda wowote.
❌ Matibabu ya ghafla – Si kila mtu ana bima ya afya, na gharama za hospitali zinaweza kuwa mzigo mkubwa.
❌ Majukumu ya kifamilia – Kuna mtu huko nje anaweza kupatwa na shida. Unaweza kumpoteza mzazi au ndugu wa karibu ukalazimika kusafiri mwendo mrefu na kutoa matumizi msibani.
❌ Kudorora kwa biashara – Ikiwa una biashara, unaweza kukabiliana na mauzo duni, wateja kuchelewa kulipa mikopo, na mabadiliko yasiyotegemewa.
❌ Mabadiliko ya kiuchumi au kisiasa – Mabadiliko ya bei, kushuka kwa thamani ya fedha, au sera mpya za serikali zinaweza kuathiri mapato yako. (Kawaida, vitu hivi huwa nje ya uwezo wako).
Unapaswa Kuweka Akiba Kiasi Gani?
____________________
Awali ya yote, kaa chini na kutambua matumizi yako ya mwezi kwa vitu muhimu: kodi ya nyumba, chakula, umeme, maji, nauli, mafuta (kama una chombo cha moto), mavazi nk. Piga hesabu, halafu tanua wigo kidogo. Kwa mfano, kama matumizi yote ni 189,500, unaweza kukadiria 200,000. (Laki 2 ndo itakuwa matumizi ya mwezi mmoja).Baada ya kutambua hilo, fanya hivi:
1️⃣ Anza na kiashi kidogo– Hifadhi angalau mwezi mmoja wa matumizi (kwa mfano wa leo, laki 2).
2️⃣ Wafanyakazi – Weka akiba ya miezi 3–6 ya matumizi yako yote (kwa mfano wa leo, itakuwa laki 6 hadi 1.2m).
3️⃣ Wafanyabiashara/wenye ajira binafsi– Hifadhi kiasi sawia na angalau miezi 6 hadi 12 ya matumizi, kwani siku hazilingani. Kiasi kinakuwa kikubwa kwa sababu unashughulikia matumizi ya nyumbani na ya biashara pia.
Kwa wanafamilia: Unaweza kulenga TZS 6M au zaidi. Maisha na majukumu hayasubiri, na mawimbi yake hayajulikani.
Hela Hizi Uzitunze Wapi?
____________________
Akiba yako ya dharura inapaswa kuwa:✅ Rahisi kufikiwa – Lakini isiwe rahisi kiasi cha kutumiwa hovyo.
✅ Salama dhidi ya mawimbi ya kiuchumi– Epuka kutunza fedha sehemu ambapo hamna usalama. (Ntakupa mbadala hivi karibuni. Tutakuja kuzungumzia UTT-AMIS, bond za serikali, na Money Market Funds (MMF) baadaye).
Unaweza kutumia:
🔹 Akaunti za simu (M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas) – Zingatia gharama za kutoa. MPESA wana products kama MGODI, MPAWA nk ambazo zinaweza kukupa riba kidogo kwa mwezi/mwana.
🔹 Akaunti za akiba benki – Chagua benki isiyo na makato makubwa. CRDB na NMB wako vizuri (ongea na afisa uwekezaji kwanza kujiridhisha).
🔹 SACCOs/Vikoba vinavyoruhusu utoaji pesa haraka
🔹 Akaunti za muda maalum (fixed deposit, miezi 3–6) – Itakusaidia unapokuwa na lengo fulani la mbeleni.
🔹 Akiba ya pesa taslimu (endapo hakuna benki karibu) – hakikisha fedha zimehifadhiwa vizuri, na uwe macho endapo noti zitabadilishwa.
🔹 Akiba ya katika madini maalum – Dhahabu ni nzuri sana katika hili. Thamani yake huwa haishuki ovyo, na haiozi (doesn't expire). Unaweza kununua kipande cha dhahabu, ukaikatia risiti, kisha ukatunza kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
Endapo kipato chako ni kidogo, fanya hivi:
____________________
💰 Tumia kanuni ya 5hadi25 – Weka 5% hadi 25% ya pesa yoyote unayopata kulingana na kipato chako.💰 Punguza matumizi yasiyo ya lazima – Epuka anasa kama kula vitu usivyohitaji, kuishi bila bajeti au kuchukua mikopo ya simu bila sababu.
💰 Uza vitu visivyotumika – Simu za zamani, fanicha, au vitu vingine vya nyumbani vinaweza kuleta pesa za ziada.
💰 Tafuta kazi ya ziada– Fikiria kazi ndogo yoyote inayoweza kukuongezea kipato.
Akiba ya dharura itakupa:
____________________
✅ Kinga unapopoteza kazi – Jua pa kuanza kazi inapoisha.✅ Kijitegemea bila mikopo – Hutalazimika kukopa kwa dharura kutoka kwa marafiki.