Jikumbusheni Historia ya Jumuia ya Wazazi (TAPA- Tanzania Parents Association)

Alphonce Kagezi

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2015
Posts
338
Reaction score
163
TAPA: Ilianzishwa 1955,ingawa vuguvugu la kuanzishwa kwa TAPA kulitokana na TANU.
Vilianzishwa vikundi vya muungano wa wazazi toka kanda ili kusimamia elimu katika shule za wazazi.
1. Mkoa wa Dar es salaam : DAPA & MAPA
2. Mkoa wa Tanga: APA
3. Mkoa wa Kageza zamani (Bukoba): KANYIGO WESTERN LAKE
4. Mkoa wa Mara zamani (Musoma): TWIBOKE

1957 Vikundi vya wazazi kutoka kanda viliunganishwa na kuwa (TAPA) ikakabidhiwa shule 233 zikiwa nawanafunzi 15,000, ndipo TAPA ikasajiriwa katika daftari na selikali ya kikoloni kwa namba 1237 yote yalitokea bada ya selikali ya kikoloni kugundua moja ya malengo ya siri ya kuanzishwaShule za wazazi ni kumfanya mtoto wakitanzania atawaliwe na mkoloni kiutawala lakini sio kutawaliwa (akili) Maana ikiwa utabaki guru kiakili utakuwa na uwezo wa kufikiri, buni njia ya kujikomboa na ukoloni(lilikuwa lengo lisilo katika makalatasi)

Majukumu yaliyoandikwa na kuwa ndio malengi ya wazi ni:-

1. Kusimamia na Kuendesha na kuratibu elimu kwa mtoto wa kitanzania.
2. Kusimamia Malezi nje na ndani ya shule kwa vijana na jamii ya kitanzania.
3. Kulinda kuhifadhi maadili na tamaduni njema za jamii ya Wanzania .
4. Kuanda viongozi wa badaye kwa ustawi wa Tanzania

TAPA: Ilisimamia vilivyo shughuli zake za wazi na za za siri ikiwa nyuma ya TANU na badaye harakati za uanzishwaji uwt zilizo asisiwa na Titi Mohammed maarufu Bibi Titi.

Hatimaye mwaka 1961 Uhuru wa Tanganyika ukapatikana.

Huwezi kuzubgumzia harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika bila kuiona TAPA,UWT,TANU YOU THREE GE kwa sasa UVCCM.

NB: Umehifadhi Historia gani? Je unaweza Ku-share na Watanzania ambao hasa kubahatika kuhifadhi chochote kuihusu Tanzania?Shiriki bila kutukana, kudhalilisha, kejeli dharau nk.

*Comments za kujenga na kuimarisha mshikamano au kuweka kumbukumbu sawa ni luksa.
 
Alphonce,
Katika Nyaraka za Sykes nimekutana na taarifa hiyo hapo chini:

Mnamo tarehe 7 Januari, 1951 mkutano muhimu sana ulifanyika katika Ukumbi wa Arnatouglo Dar es Salaam.

Baada ya mwaka mmoja ofisini kama katibu, Abdulwahid aliwasilisha taarifa yake kwa mkutano mkuu.

Hii ilikuwa tofauti ukilinganisha na uongozi uliopita wa wazee.

Akiangalia nyuma mwaka wa 1950, Abdulwahid aliwataarifu wanachama kuwa mwaka huo ulikuwa mgumu kwa TAA vile vile.

Wanachama walijulishwa kuhusu mwanasheria kutoka Bermuda, Earle Seaton kama mshauri wa TAA wa sheria na mchango wake katika kutayarisha mapendekezo iliyowasilishwa kwa Gavana Twining.

Wanachama walijulishwa kuhusu kufufuliwa kwa matawi ya TAA, mawasiliano yake na Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa na uhusiano ulioanzishwa na TAA na wajumbe Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria.

Abdulwahid aliwaeleza wanachama juu ya ziara yake ya Nairobi aliyofanya mwezi Oktoba, 1950, na kukutana kwake na Balozi wa India katika Afrika ya Mashariki.

Vilevile aliwaeleza kuhusu mshikamano ulioanzishwa kati ya TAA na KAU; na kutolewa nafasi za kusoma katika vyuo vikuu vya India na serikali ya nchi hiyo kwa Waafrika wa Tanganyika kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya India.

Abdulwahid alieleza kwa ufupi juu ya kuundwa kwa African Parents Association kwa msaada wa Dr Raymond na European Parents Association.

(Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January, 1951. Sykes' Papers).
 
Back
Top Bottom