Uchaguzi 2020 Jimbo la Meatu linawindwa sana na CHADEMA

Uchaguzi 2020 Jimbo la Meatu linawindwa sana na CHADEMA

Kilimbatz

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
4,331
Reaction score
5,865
Kama kuna jimbo ambalo CHADEMA wanaliwinda kwa udi na uvumba basi la Meatu lipo juu kwenye list!

Ni jimbo ambalo lilikuwa chini ya CCM likiwakilishwa na mfanyabiashra mwenye kiwanda cha vintwaji JAMBO kilicho mkoani Shinyanga
Jimbo kwa sasa lina wagombea wawili Leah Komanýa wa CCM na Mwl Johston wa CHADEMA

Ugeni pekee wa kitaifa wa CCM uliofika hapa Meatu kukiombea chama cha CCM ni Mhe Kasim Majaliwa pekee huku uongozi wa juu wa CHADEMA ambao ushafika huku ni Salum Mwalim na Tundu Lissu

Na leo kwa mara ya pili tena Mgombea mwenza Salum Mwalim anakuja tena Meatu

Je kutokukubalika kwa Leah Komanya kwa watu waliokuwa watiifu kwa Jambo ndiyo kunawafanya CHADEMA waamini kuwa wanaweza kulichukua jimbo hili au kuna kingine?

NB:Meatu ndiyo wilaya pekee ambayo mawakal wote wa CHADEMA wameapishwa na na katika kata kumi na sita za jimbo lote.
Kwanini Salum Mwalimu anarudi tena huku Meatu?

Pichani Salum Mwalimu akiwa Maswa akielekea Meatu.


Screenshot_20201023-121200_Twitter.jpg

 
Niko na Luzibukya hapa, tuna kampeni yetu nyumba kwa nyumba! Kwa siku tunapita nyumba 100, ccm hapa meatu imeshapukutika!
Wanameatu wanasema 28/10/2020 wanajbo lao!!
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndio inapanga ratiba.

Lakini ukiangalia kampeni za Chadema maeneo aliyopita mgombea Uraisi, lazima mgombea mwenza apite.

Je, umeangalia ratiba za wagombea wa vyama vingine na kujiridhisha kwamba na wenyewe hawakupangiwa kupita Meatu mara nyingi kama ilivyo kwa Chadema?

Kanda ya Ziwa ni ngome ya CCM, lakini Chadema hawatakiwi kuacha kukampeni ktk ukanda huo.
 
Back
Top Bottom