Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
Naomba nilizungumze hili kwa moyo wa dhati kabisa na kwa mapenzi makubwa kabisa ya chama changu. Bado tunaamini kwamba chama chetu hakijapata mbadala wake na bado hakuna dalili hizo kwa maneno ya mzee wangu makamu mkuu wa chuo cha UDSM Prof Mukandara.
CCM chama changu pendwa, kuna malalamiko makubwa sana ya wananchi na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Ikungi kwamba aliyekua Mbunge wa jimbi hilo ndugu Elibariki Kingu anagawa rushwa kwa kila mjumbe hivi sasa ili aweze kupigiwa kura za kishindo. Haya si maneno yangu ni ya wajumbe wenyewe na mkitaka kujua fanyeni uchunguzi muone ukweli ulivyo. Mtu huyu anasaidiwa kufanya kazi hii na mwenyekiti kiti wa Wilaya ndugu Mika Likapakapa. Wananchi wana hasira sana na vitendo hivi na kiukweli kabisa wameapa kupiga kura za hasira kwa upinzani ili kumkomesha kwa vile hawamtaki kabisa.
Nayazungumza haya siyo kwa nia mbaya bali ni kwa maslahi mapana ya chama changu, jimbo na taifa kwa ujumla.Sina chuki yeyote wala hiyana na mbunge huyu mstaafu ila amefanya chama kichukiwe sana na wananchi kutokana na kutotimiza ahadi zake zote za mwaka 2015 alizotoa wakati wa kampeni. Kuna shida kubwa ya Maji, Umeme, miundombinu, Afya na Elimu ambapo mashule mengi madarasa hayana madawati jimboni humo. Twafahamu kua yeye hawezi kujenga kwa pesa zake mwenyewe, basi awsemee wananchi hawa ili serikali iwaonee huruma. Yeye amekua akisemwa kua siyo mkweli muda wote anatoa ahadi hewa.
Inasemekana vyama vya upinzani jimboni humo vinategea arudishwe na chama wataungana kwa kuweka mtu mwenye nguvu anayependwa na watu wengi waweze kumuondoa. Hili linawezekana kabisa chonde chonde chama changu nakipinda tusifanye kosa tunaangalia kwa macho.
Inasemekana pia ikiwa kweli Tundu Lisu atagombea Urais mwaka huu upepo wake unaweza kubadilika na tukapoteza majimbo yote mawili ya Magharibi na mashariki. Jimbo la Mashariki wananchi wanadai kua Mbunge aliyepo sasa ndugu Miraji Mtaturu hana mvuto wa kisiasa na pia hamudu majukwaa ya kisiasa vizuri. Huko pia tukiwekewa na upinzani mtu mwenye nguvu anayejua kusema vizuri tunaweza kupoteza jimbo kwa mara ya tatu sasa. Inasemekana naye anagawa rushwa kwa kiasi kikubwa sana kujihakikishia ushindi kwenye kura za maoni.
USHAURI WANGU
Haya yote yanafanyika kwa sababu ya udhaifu na uzembe wa Mwenyekiti wa Wilaya ndugu Mika Likapakapa. Ndiye inasemekana anasuka mipango yote ya rushwa na haelewani kabisa na timu ya viongozi wengine wa Wilaya.Menyekiti huyu aondolewe kwenye nafasi yake na ikaimishwe. Tutakuja kukumbuka maneno yangu haya huu ushauri ni kwa nia njema kabisa kwa chama changu. Tumelalamikia mitendo hivi ngazi mbali mbali za chama kuanzia mkoa hadi taifa tunaona kimya tu. Tusije tukajutia na atutaki kujutia kwa hili wakati tunaangalia na twajua