GE2025 Jimbo la Temeke lagubikwa na rushwa, vitisho na ukiukwaji wa maadili ya chama ktk kura za maoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

KIJICHO PEVU

Member
Joined
May 4, 2024
Posts
69
Reaction score
49
Na Mwanachama Hai wa CCM TEMEKE

Utangulizi
Kwa masikitiko makubwa na kwa dhamira ya dhati ya kulinda heshima, maadili, na misingi ya haki ndani ya chama chetu, napenda kuwasilisha taarifa hii maalum ya uchunguzi wa awali kuhusu mchakato wa kura za maoni ndani ya Jimbo la Temeke. Taarifa hii inaonesha namna mchakato huo uligubikwa na matumizi makubwa ya fedha haramu (rushwa), vitisho kwa viongozi wa ngazi za chini, upendeleo wa wazi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa wilaya, na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi wa ndani wa chama.

Hali hii, ikiwa haitachukuliwa hatua stahiki, si tu inahatarisha mshikamano wa wanachama, bali pia inalifedhehesha na kulidhoofisha chama chetu mbele ya wananchi na wapigakura waaminifu.

1. Matumizi ya Rushwa kwa Shabaha ya Kulazimisha Ushindi

Mgombea mmoja, Mariamu Kisangi, ameripotiwa kutumia zaidi ya Tsh 100,000,000 kwa minajili ya kushawishi viongozi na wajumbe kuhakikisha anashinda kwa lazima. Mifano halisi ni pamoja na:

Kutoa Tsh 30,000,000 kwa Katibu wa Wilaya kama hongo ya kuungwa mkono.

Kumfadhili Mwenyekiti wa Wilaya na wajumbe wa sekretarieti kwa mamilioni ili kuendesha kampeni ya kimya kimya ya kumtangaza yeye pekee.

Kumpa kila Katibu wa Kata kiasi cha Tsh 5,000,000, kwa masharti kwamba wasimamie ushindi wake kwa gharama yoyote ile.

Jambo hili liligeuza mchakato wa kura kuwa mnada wa uongozi, si kigezo cha uwezo au ridhaa ya wanachama.

2. Uendeshaji Usio wa Haki kwa Kushirikisha Viongozi wa Kata na Matawi

Katika Kata kama Makangalawe, Buza, na Vituka, wenyeviti wa kata walishirikiana hadharani na mgombea Mariamu Kisangi katika kutoa rushwa na kusimamia kupindisha matokeo. Hili ni tusi kwa wapigakura halali na wanachama waadilifu waliokuwa wakitegemea haki itatendeka.

3. Vitisho kwa Viongozi wa Ngazi za Chini

Viongozi waliokataa kushiriki njama za rushwa walitishiwa kwa maneno na vitendo. Mfano unaoumiza zaidi ni wa:

Bi. Rhoda, Katibu wa Tawi la Machimbo – Yombo Vituka, ambaye aliitwa wilayani na kutishwa hadharani baada ya mgombea Kisangi kushindwa kupata kura za kutosha.

Licha ya kuteuliwa kama wakala wa usimamizi wa kura, alijikuta akibeba mzigo wa lawama kwa sababu tu mgombea huyo alipata kura 83, huku Fadhili Famonga akiongoza kwa kura 632 katika kata hiyo.

Vitisho hivi vimewavunja moyo viongozi wengi wa chini na kudhoofisha ujasiri wa kusema ukweli ndani ya chama.

4. Uchakachuaji na Uchezewaji wa Matokeo

Baada ya kushindwa kwenye baadhi ya kata, Katibu wa Wilaya aliamuru matokeo yazuiliwe, huku akitoa maelekezo ya kuyapitia upya kwa usiri mkubwa. Katika hali ya kustaajabisha:

Kata kama Mtoni na Azimio ziliwekwa mwisho kimakusudi.

Umeme ulizimwa mara kwa mara, hali iliyowawezesha baadhi ya mawakala kupenyeza kura zisizo halali.

Mgombea Mariamu Kisangi na timu yake walikusanyika kwenye ofisi za chama Wilaya huku wakihesabu tena kura kwa utaratibu wa kivuli.

Tukio hili linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote, kwani ni tisho kwa demokrasia ya ndani ya chama.

5. Ushirikishwaji wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa Upendeleo

Taarifa za kuaminika zinathibitisha kuwa Mkuu wa Wilaya alihusishwa moja kwa moja, akipokea fedha kutoka kwa Mariamu Kisangi ili Askari wa usalama wapewe maelekezo ya upande mmoja, kwa lengo la kuzima malalamiko au upinzani kutoka kwa wapiga kura na wagombea wengine.

Hili ni jambo la hatari kwa ustawi wa chama na kwa mustakabali wa nchi, ambapo vyombo vya dola vinaweza kuingizwa kwenye siasa za upande mmoja.

Hitimisho: Wito wa Hatua Haraka
Ni dhahiri kuwa mchakato wa kura za maoni Jimbo la Temeke umechafuliwa kwa kiwango cha kutisha. Rushwa, vitisho, upendeleo na ukiukwaji wa taratibu zimepelekea uongozi kupoteza uhalali wa kimaadili na kisiasa.

Mapendekezo:
1. Tume huru ya chama ichunguze kwa kina mchakato wa kura Temeke.
2. Viongozi waliotajwa wapelekwe kwenye Kamati ya Maadili mara moja.
3. Matokeo yasitishwe rasmi hadi uchunguzi huru ukamilike.
4. TAKUKURU na vyombo vya dola wachunguze mwenendo wa fedha na ushiriki wa viongozi wa serikali.
5. Viongozi waliotishwa walindwe kisheria na kisiasa dhidi ya manyanyaso yoyote.

Mwisho
Rushwa haijawahi kuwa njia ya haki, na ushindi unaopatikana kwa hila ni fedheha kwa taifa na chama. Chama makini hakiwezi kufumbia macho kilichoendelea Temeke. Ni wakati wa kufanya maamuzi ya kihistoria: kulinda heshima ya wanachama au kuendelea kulia kimya kimya huku haki ikizikwa kwa noti.
 
Kilave amepewa nafasi ameishia kuichezea kwahiyo asitegemee kurudi Bungeni huyo Mchaga mwambie hajitambui
 
Watu hawa hawa ndio huwa wanawanyooshe vidole upinzani wakati vidole 3 wikimwangalia
 
Ubunge wa CCM haupatikani kwa lele mama.

Pia hakuna mgombea anayepita kura za maoni bila kuwapa takrima wajumbe wake,,,

Mtoa mada umezidiwa maujanja ndio maana unalalamika.

Kwanza kama huyo mariam katumia milioni 100, ujue ni mjanja sana. Milioni 100 ni hela ndogo sana kwenye kushinda kura za maoni za ccm.
 
Tume huru tena, tangu lini imekua huru?
TAKUKURU wanashughulika na rushwa ndogo ndogo.
Umeshawahi kuona takukuru wakimkamata mtu aliyetoa rushwa ya milioni mia.
Hiyo ni above their scope. Takukuru waambie mwalimu mkuu amechukua rushwa ya elfu kumi toka kwa mzazi wa mwanafunzi. Hapo utawaona wakifanya kazi.
Mbona baiskeli, pikipiki hubiongelei?
TA
 
Uki staajabu ya TEMEKE Utayaona ya MBEYA.

UBUNGE VITI MAALUMU UNA NUNULIWA.

Haki ya Uwakilishi Imenunuliwa
Haki ya Kundi Maalumu la Wanawake kumbe wanajiweza ikiwa kama watauza nafasi na Kununua Nafasi.

Ubunge wa VITI MAALUMU MBEYA Umefika bei sio Uwakilishi Tena Bali ni Biashara.
Aibu Kwa CCM naona mimi Mpita njiaa.
 
Acha kelele wewe!! hata wewe ulitoa mlungula sema bi Mama kakuzidi,so hiyo sio HOJA ..labda hiyo ya viongozi kutishiwa ila una ushahidi tangible or kelele tu baada ya kugalagazwa?...CCM na RUSHWA ni Chanda na Pete ..yaani kama mmerogwa vile
 
Du! Inaonekana huyo Mariam Kisangi mtu wa mbungi sana, yaani mambo yote anafanya yeye.

Kuna watu waliapa liwake jua inyeshe mvua mjengoni lazima waingie that's why wanaspend pesa nyingi sana.
 
October mnatick au SIYO?
Pole mkuu kwa kuzidiwa nguvu, TUME HURU YA UCHAGUZI HAIHUSIKI NA MCHAKATO WA KURA ZA MAONI ZA VYAMA VYA SIASA
 
Acha kelele wewe!! hata wewe ulitoa mlungula sema bi Mama kakuzidi,so hiyo sio HOJA ..labda hiyo ya viongozi kutishiwa ila una ushahidi tangible or kelele tu baada ya kugalagazwa?...CCM na RUSHWA ni Chanda na Pete ..yaani kama mmerogwa vile
Nakuona Katibu UWT MBEYA AMINA MWIRU.

Yaani Mgombea akunulie Gari Una jisahau kabisa kuwa Umeuza Nafasi ya Uwakilishi??!!.

MBEYA HAPO muda huu AMINA MWIRU Katibu Anakula faida mara baada ya FYANDOMO kulipa gari na kama zawadi kusaidia kwenye kinyang'anyiro cha Uwakilishi Wanawake Mkoa Mbeya.

Aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…