Kutoka kwa Mdau
=====
Je, ni kweli Jimbo la Texas lilinunuliwa na Marekani kutoka Canada Mwaka 1920?
=====
Je, ni kweli Jimbo la Texas lilinunuliwa na Marekani kutoka Canada Mwaka 1920?
- Tunachokijua
- Texas ni moja ya majimbo makubwa zaidi nchini Marekani, likiwa na eneo kubwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 30 kufikia mwaka 2023. Jimbo hili linapatikana kusini mwa Marekani, likiwa linapakana na Mexico upande wa kusini.
Je, ni kweli Jimbo la Texas lilinunuliwa na Marekani kutoka Canada Mwaka 1920?
JamiiCheck.Com imefatilia Historia ya Jimbo la Texas na kubaini kuwa historia ya Texas kununuliwa na Marekani Mwaka 1920 haina ukweli wowote kwani Mwaka 1920 Texas ilikuwa tayari ni moja ya majimbo ya Marekani mbapo ilijiunga na Marekani Mwaka 1845, Pia kwenye historia, Texas haijawahi kuwa chini ya utawala wa Canada. Historia ya Texas inahusiana zaidi na Uhispania, Mexico, na Marekani, na Si Canada.
Vilevile, Kijiografia Jimbo la Texas linapakana na nchi moja tu jirani nayo ni Mexico, na Mpaka huu uko upande wa kusini wa Texas. Katika pande zake nyingine Texas inapakana na majimbo mengine ya Marekani kama Louisiana kwa upande wa mashariki, Arkansas kwa upande wa kaskazini-mashariki, Oklahoma kwa upande wa kaskazini na New Mexico kwa upande wa magharibi.
Canada haipakani na Texas kwa upande wowote, nchi pekee inayopakana na Texas ni Mexico.
Historia inaonesha miaka ya 1519 hadi 1821, Texas na Mexico zilikuwa chini ya himaya ya Uhispania. Ambapo mwaka 1821, Mexico ilipata uhuru kutoka Uhispania na kuwa nchi huru, huku Texas ikiwa ni sehemu ya Mexico.
Baada ya Mexico kupata uhuru kutoka kwa Uhispania na Texas kuwa sehemu ya Mexico. Texas ilikuwa jimbo la kaskazini mashariki mwa Mexico, lakini kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya wenyeji wa Texas na serikali ya Mexico, hasa kuhusu sheria za mali, dini, na utawala.
Mnamo 1836 Texas ilipata uhuru kutoka kwa Mexico baada ya Mapinduzi ya Texas kufuatia Vita vya Alamo na San Jacinto. Kwenye vita hiyo Texas ilishinda na kupata uhuru ambapo Jamhuri ya Texas ilitangazwa na ikawa nchi huru kwa miaka 9. Baada ya Texas kuwa huru, Mexico haikuwahi kuitambua rasmi kama taifa huru, ikidai kwamba Texas bado ilikuwa sehemu ya Mexico. Aidha, Texas ilikuwa na uhusiano wa karibu na Marekani.
Baada ya miaka 9 Texas kuwa huru, mnamo Mwaka 1845, Texas iliunganishwa rasmi na Marekani na kuwa jimbo la 28 la Marekani.
Aidha, Baada ya 1845 Texas kujiunga na Marekani, kulisababisha Vita kati ya Marekani na Mexico mnamo 1846–1848 kwa kuwa Mexico haikuridhia kuwa Texas ilikuwa nchi huru, Mexico ilikuwa inadai Texas bado ni sehemu ya Mexico na kuona kama Marekani wameinyakua.
Aidha, kwenye Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani, Mwaka 1861, Texas ilijitenga na Muungano wa Marekani na kujiunga na Muungano wa Kusini (Confederate States of America)
1865 Baada ya kushindwa kwa Muungano wa Kusini kwenye Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani, Texas ilirejea tena kuwa sehemu ya Marekani n kuendelea kuwa Sehemu ya Majimbo ya Marekani mpaka sasa mwaka 2024.