PreGE2025 Jimboni kwa Bashe moto unawaka anapumulia mashine

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Shakari

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2022
Posts
211
Reaction score
629
HALI ya kisiasa jimboni Nzega Mjini kwa Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe ni mbaya tofauti kutokana na kutokubalika na wananchi licha ya kutumia fedha nyingi kugawa kwa wajumbe na baadhi ya viongozi ili kumpigania ashinde kura za maoni.

Suala la uzawa nalo linamtesa wakikumbushia mambo ya 2010 wakati wa Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu utata wa uraia wake anatajwa mtu mmoja anaitwa Mashili kama mpinzani wake mkuu licha ya kuwa hana fedha kumzidi Bashe ila anaonekana kukubalika sana kwa wananchi.

Licha ya Bashe kuwahonga viongozi wote wa vijiji, kata na matawi wa Chama cha Mapinduzi fedha nyingi na kuwapatia pikipiki lakini bado hazijamsaidia kumuongezea sifa kwa wananchi na kuzalisha mpasuko mkubwa ambapo wananchi wa kawaida wapiga kura ambao hawajepewa pikipiki nao wanaweka shinikizo kuwa nao wapewe pikipiki ndipo washiriki uchaguzi.

KWA mujibu wa sensa Nzega inakadiriwa kuwa na watu 115,193 hivyo wananchi wote hao nao wanataka wapewe pikipiki kila mmoja ndiyo wafikirie kumuunga mkono Bashe
 
Kama Rais na mwenyekiti wake kagawa pikipiki nchi nzima,Bashe nae atagawa tu Jimbo zima,hata baiskeli moja moja kwa mfumo qa fedha,CCM hushindana kwa uchafu,hakunaga msafi!!
 
Hao watu 115,193 ni wapiga kura wa jimbo la nzega au ni wanchi wa nzega.
kama ni wapiga kura sawa kama ni wananchi hiyo hesabu sio sawa.
 
Hivi mambo kama haya takukuru huwa hawahusiki?


Bashe agawa pikipiki zipatazo 229 zenye thamani ya takribani Milioni 700 kwa viongozi wa Chama na jumuiya zake katika ngazi ya kata na matawi, pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Mitaa, katika Jimbo la Nzega mjini.
 
View attachment 3297793

Bashe agawa pikipiki zipatazo 229 zenye thamani ya takribani Milioni 700 kwa viongozi wa Chama na jumuiya zake katika ngazi ya kata na matawi, pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Mitaa, katika Jimbo la Nzega mjini.
Kwa huu uwekezaji kuna mtu atakubali reform kwel?🤔
 
Mashili acha huu ujinga wa kuja kujipigia campaign JF, hakuna mpiga kura wako humu.
 
Siasa ni mchezo mchafu huyo mashili ni upepo Tu wa mwanzo subiri uchaguzi wenyewe ufike utamuona Tu bashe huyoo mgombea tena wa jimbo la nzega mjini na atakua waziri tena this is Tz
 
Mashili acha huu ujinga wa kuja kujipigia campaign JF, hakuna mpiga kura wako humu.
Hiyo haiondoi ukweli kwamba Bashe ni mtu mbaya sana wanapora mali za nchi kupitia uzalendo wa kitapeli. Sio hilo tu pia Bashe anakwamisha maendeleo ya Nzega kwa sehemu kubwa sana. Nitakupa facts chache.

Huyo Mashili alijitolea kujenga barabara za mtaa uzunguni karibu na hospitali. Akawasiliana na TARURA ili walete wataalamu na Mashili alete materials yote kupitia kampuni yake. Bashe akazuia kwa madai ya kipuuzi kabisa kwamba serikali haijakosa fedha za kujenga. Zile barabara hazijajenga mpaka leo. Amekuwa akifanya hivyo kwa wafadhili wengi wana Nzega wakitaka kujenga miundombinu au kutoa msaada. Za ndani ni kwamba anahisi hao watu wanataka kugombea.

Bashe ameiba fedha za BBT akaenda kujenga mradi mkubwa wa kilimo wa zaidi ya bilioni 5 Uyui katikati ya barabara ya Tabora na Nzega. Kwa wasivyo na aibu ameutenga barabarani tu.

Bashe amekuwa akikwamisha uuzaji wa choroko stakabadhi gharani kwa kupokea mihela kwa wanunuzi. Badala yake wakulima wanauza mazao kwa bei isiyo shindani.

Sasa utasemaje Bashe mzalendo
 
Hizo barabara hazikuwa zinasumbua kipindi cha nyuma..? Mashili kwanini hakuzirekebisha kipindi hicho? Anyways, hata kama una nia njema ila ukishaonesha nia ya kutaka jimbo, huwezi kupewa support ya kufanya jambo kama hilo. Simlaumu Bashe kwa kutetea jimbo lake, ni Mwanasiasa na yeye.

2. Bashe sidhani kama kaiba hizo hela, report ya CAG isingemuacha salama. Labda kama una ushaidi zaidi ambao serikali hauwezi kuupata. Na ushahidi wa aina hio sidhani kama una afya kwa taifa, hatuwezi kumuwajibisha yeyote kwa ushahidi usio wazi.

3. Stakabadhi gharani sio mradi wa bashe, nenda kapitie sera za kilimo za taifa alafu uone kama ni yeye au sera ndo inasema.

Anyways, me simtetei Bashe, i hardly know him ila hoja zenu hizo nyepesi sana na zimekaa kisiasa zaidi. Bashe ni mwanasiasa mzuri sana, atawashinda mchana kweupe kwa hoja hizo. Last election ya kura za maoni, Bashe nadhani alitangazwa saa 8 mchana, do you know what that means..? Huyo mtu ana ushawishi mkubwa sana.
 
Mimi sizungumzii habari ya Bashe kushinda, kwa sababu sio mjinga nisiyejua CCM wanashindaje. Nazungumzia mnachokiita Bashe ni msafi. Bashe ni walewale tu wanaokunywa uji wa mgonjwa Tanzania.
2. Athibitishe ametoa wapi fedha zote hizo
3.Sijui hata wewe unaelewa umeandika manini.
 
Nzega nao wajinga sana, watu wanatoka Somalia huko wanakuja kuwatawala! Watz wanahitaji kuamka usingizini na kujitambua ipasavyo.
 
Yaani wewe jamaaa yaani mashili amshinde BASHE???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…