Jina halionekani kwenye list ya chuoni ila NACTE lipo

wejja

Senior Member
Joined
Nov 1, 2011
Posts
126
Reaction score
16
Salamu wakuu,
Mimi ni mhitimu wa kidato cha nne wa mwaka 2013 na nilituma maombi ya kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada (hisabati/sayansi) na nilibahatika kuchaguliwa katika chuo kikuu cha Dodoma (Udom) katika program maalum. Kwa mara ya kwanza niliona jina langu kupitia website ya NACTE nikiwa miongoni mwa waombaji wengine zaidi ya 4000 tuliochaguliwa katika chuo hicho, majina hayo yalitangazwa tarehe 14 September mwaka huu. Lakini majina yaliyotolewa na chuo (UDOM) tarehe 29 September (juzi) jina langu halionekani.
Naombeni msaada jamani maana furaha yangu imepukutika ghafla.
 
kama yaliyotoka ni kwa batch basi subiri batch zinazofuatia usihofu jina lako lipo tu
 
Wasiliana na admision ofice udom wao watakupa majibu ya uhakika tafuta namba zao ktk website yao kesho uwasiliane nao
 
Thanks a lot mkuu manuru
 
Salamu wakuu,
Mimi ni mhitimu wa kidato cha nne wa mwaka 2013 na nilituma maombi ya kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada (hisabati/sayansi) na nilibahatika kuchaguliwa katika chuo kikuu cha Dodoma (Udom) katika program maalum. Kwa mara ya kwanza niliona jina langu kupitia website ya NACTE nikiwa miongoni mwa waombaji wengine zaidi ya 4000 tuliochaguliwa katika chuo hicho, majina hayo yalitangazwa tarehe 14 September mwaka huu. Lakini majina yaliyotolewa na chuo (UDOM) tarehe 29 September (juzi) jina langu halionekani.
Naombeni msaada jamani maana furaha yangu imepukutika ghafla.

Nipe jina lako nikuangalizie pengine yawezekana uliangalia kwa kiwewe!
 
wala usihofu wejja kila kitu kipo sawa mkuu majina ya batch nyingine yapo njiani
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom