jMali
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 8,404
- 4,973
“Hakuna mwekezaji atawekeza kwenye nchi ambayo kesi ikipelekwa hapo Kisutu kiongozi yoyote anaweza kupiga simu akaielekeza mahakama nini cha kufanya.” –Rostam Abdulrasul Aziz, June 26 2023.
Angalizo: Bahati hii haihusishi Maazizi wote, sio wewe Aziz Ali wa Mtongani wala Aziz ki! Usijichanganye ukafanya wanayofanya hawa Maazizi utafia jela.
Mwaka 2011 Ndugu Assad Aziz Abdulrasul alikamatwa akituhumiwa kusafirisha kilo 92 za Heroin kutokea Iran. Kesi ilipoenda mahakamani kukatokea maajabu. Assad akapewa dhamana! Yalikuwa ni maajabu kwani Mahakama yenyewe haikuwa hata na uwezo wa kusikiliza hayo mashtaka, ni zile mahakama za chini ambazo kesi inatajwa tu ikisubiri kupelekwa Mahakama kuu! Lakini hata huko Mahakama kuu makosa yaliyomkabili bwana Aziz yalikuwa hayana dhamana vile vile!
Kwenye kesi kubwa kama hii ya Madawa ya kulevya ambayo haina dhamana Hakimu “alikosea” akatoa dhamana fasta, na upande wa Jamhuri hawakuona tatizo, ila kwenye kesi za kina Boni yai ambazo zina dhamana, Hakimu anakuwa “makini” sana hataki kukosea hivyo Boni Yai anaenda kusota jela kwa kosa lenye dhamana wakati Hakimu “anafikiria” hoja za Jamhuri. Talk about “Mahakama za Juma!”
Kesi ilipofika huko Mahakama kuu Assad (aliyekuwa anakula bata nje kwa dhamana) akaachiwa huru kwa kile ambacho Hakimu alisema ni kuborongwa kwa ushahidi wa Jamhuri! Hakuwa na kesi ya kujibu, wale wenzake wote ambao walikutwa na kesi ya kujibu pia baadae wakaachiwa! Fikiria kesi ya kilo 92 ambazo watu wamekamatwa nazo “laivu”, lakini somehow they walked! Jamhuri ‘ilisahau’ kuleta vielelezo muhimu, hivyo kesi ikawa haina nguvu.
Mwaka 2018 ambapo Aziz mwingine, bwana Akram Aziz alikamatwa kwa makosa mbalimbali kuhusu uwindaji haramu. Picha za vidhibiti tulizoonyeshwa zilionyesha pembe za ndovu,silaha nyingi sana za kuwindia n.k, polisi wanasema Akram pia alikutwa na mihuri bandia na vibali bandia vya kuwindia. Lakini iliyofunguliwa Mahakamani haikuwa na Pembe za Ndovu ikawa kesi ya nyama kilo 65 za Nyati za thamani ya milioni 4 na silaha, hivyo kesi ikawa na option ya kulipa fidia, akalipa akatoka! Yale meno na makorokoro mengine sijui mihuri, vibali nini nini tuliyoonyeshwa kwenye picha sijui Jamhuri ilipeleka wapi. Bwana Akram Aziz akaachiwa huru!
Mwaka jana Oktoba, Aziz mwingine, Assad Abdulrasul Aziz alikamatwa yeye na wenzake kwa utekaji wa binti wa Mfanyabiashara mkubwa, ambapo walikaa naye siku 4 wakiwa wanataka walipwe dola milioni 3.5 za marekani. Polisi waliwakamata wakiwa na gari waliyotumia kumteka bi Hani Nooh Hussein, pamoja na Bastola waliyotumia kumtishia maisha.
Ila sasa, amini usiamini eti DPP akaona kuna haja ya kuingia makubaliano kwenye kesi straight-forward kama hii yenye ushahidi wa kutosha. Makubaliano yakawa wakubali kosa moja tu la utekaji halafu waende jela miaka 3.
Kisheria, kama kuna makubaliano ya DPP na mtuhumiwa (plea bargain), basi Mahakama inachukua makubaliano yale kama ndio hukumu yenyewe. Kwa hiyo ilitakiwa Assad Aziz aende jela kutimiza masharti ya Plea bargain.
Nukuu ya plea bargain yenyewe inasomeka:
’12. The accused persons agree to plea the offence of Abduction with intent to confine and each accused is ready to serve three years in jail.
19. The Court shall sentence to each accused person to serve three years in jail.”
Kufika Mahakamani, Hakimu A.M Lyamuya (TLS watusaidie tumjue, mwamba kabisa huyu). “akakosea” na badala ya kuchukua makubaliano ya plea bargain, yeye akatoa maamuzi yake alikojua yeye ya kwamba washitakiwa walipe shilingi laki tatu (300,000 tzs). Ndio, yani watu sita wamteke binti wa watu, wamfiche siku 4 huku wakidai fedha bilioni zaidi ya 7 kutoka kwa wazazi wake, wakikiri hilo kosa adhabu yake ni shilling laki 3! Aziz Abdulrasul Aziz na wenzie wakaachwa huru!
Uamuzi huu ulisababisha wazalendo serikalini kuandika barua Mahakama kuu ya kuomba mapitio maana uamuzi ulikuwa wa hovyo kabisa. Mahakama kuu imeamua kufuta huhumu hii ya Lyamuya na kumtaka DPP wawakamate watuhumiwa upya ili waende jela kutumikia kifungo walichokubaliana kwenye plea bargain.
Je unadhani mtekaji Assad Abdulrasul Aziz yuko nchini? Unadhani Tanzania itaandika barua nchi aliyopo (Interpol etc) ili arudishwe kutumikia kifungo chake cha miaka 3 jela? Mimi nadhani kwa “bahati” tu alivyotoka alienda straight nchi ambayo haina extradition treaty na Tanzania, ila ni mawazo yang tu, labda itatokea akawa hapo hapo Masaki, tuulize DPP na Polisi maana uamuzi wa Mahakama umetoka majuzi tu hapa.