Jina la Yesu lina TBS kuzidi majina mengine yote

Je huyo ndio Mungu? Una uthibitisho gani usio wa kinadharia ku prove hilo... Yaani nijue ya kuwa kitu kinacho nifanya nipumue ni Mungu?
hakuna uthibitisho unafikiri kama mungu hayupo yupo nan anayefanya jua lichomoze na kuzama?
 
Basi umwage hadhani leo nijue. Maana imekuwa siri kwa karne na karne
Tangu kuzaliwa kwangu hadi leo nina mengi ya kushuhudia. Nilikuwa mdadisi sana utotoni kuhusu uwepo wa Mungu, Yesu na Roho wa Mungu.
Nilichoambulia mpaka sasa ni uthibitisho wa uwepo huo mkuu, Mungu hunipa new dawn kila ninapokutana na mlima kwenye maisha.

Mtazamo wangu na Imani yangu kuhusu Yesu haiko based kwenye misingi au mwelekeo wa kidini. Mungu ni Mkubwa na Uweza Mkuu zaidi ya hizi dini zinazojipa mamlaka kuwa ndiyo sauti, misimamo na maamuzi yake.

Kwa mara nyingi ameninyakua kutoka ktk kifo. Nilipaswa kufa tangu nikiwa kijana mdogo. Nikiwa na umri wa miaka 11 nilioneshwa kuwa kuna ajali ya kukatwa jembe la kichwa, nikawaeleza wazazi wakapuuzia mchana wake nikapatwa na hiyo ajali...... madaktari Muhimbili walishindwa kuamini niliwezaje kuwa hai hadi wananishona.

Nina mengi sana ndugu yangu ya kuthibitisha Upendo, Ukuu, Uweza na Uwepo wa Mungu ambaye ni beyond na ufahamu, akili na uwezo wetu.

Ukifuatilia threads kunihusu humu, utagundua mwaka jana nilipatwa na Kiharusi kikali sana. Upande mmoja wa mwili kuanzia miguuni hadi kichwani kuliathirika. Nilikuwa siwezi lolote yaani kuongea, kutembea, kuandika, kutafuna na mwili ulikuwa ktk maumivu makali sana hata nipige kelele vipi naishia kutoa sauti ya kukoroma. Lakini hapa ninapoandika nipo kwenye mikoa yenye baridi kali sana nimevaa pensi na tshrit nikikujibu swali lako. Yaani nimepona na kuimarika.

Nimemtafakari sana Yesu, nimeona wengi wanamuelewa kwa mwelekeo wa kidini. Wengine wamejiaminisha wanammiliki Yesu wakati sivyo kabisa.

Need me to say more?
 
je tukikuambia kila kitu tatizo ni kipofu ...sasa kama jina la yesu lina nguvu hatujakataa mbona kaja halafu hamjamkubali ? kaja na jina jipya ka update oya karibu katika ufalme wa Mungu .....jina jipya la kristo ni Olumba Olumba Obu
 

Attachments

  • FB_IMG_1783846562065.jpg
    80.8 KB · Views: 11
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…