Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
JINA LAKE KAMILI NI JUMBE SHOMARI JAHAZI
Picha hiyo hapo chini ni picha maarufu sana.
Katikati ni Abushiri bin Salim Al Harith, wa kwanza kushoto ni Jahazi na kulia ni Makanda bin Mwinyimkuu.
Vitabu vyote vya historia vinatambulisha Jahazi kwa jina moja tu la Jahazi.
Leo kitukuu chake Jahazi kawasaliana na mimi na kaniuliza maswali kuhusu historia zaidi ya huyu babu yake mkuu ambae kanieleza jina lake kamili ni Jumbe Shomari Jahazi.
Kanifahamisha kuwa Jumbe Shomari Jahazi akiishi Winde kijiji kabla ya kufika Sadani na kipo pwani kabisa.
Kijiji hiki alikoishi Jahazi hakipo kabisa kwa sasa kilichobakia hapo ni makaburi.
Fikra yangu ni kuwa wakazi wa kijiji hiki waliondoka hapo kukimbia vita vilivyokuwa vikiendelea baina ya Wajerumani na Bushiri bin Salim ambae Jumbe Shomari Jahazi alikuwa mshirika wake.
Jahazi hakukamatwa na Wajerumani na inasemekana alikimbilia Uganda ambako aliishi hadi kifo chake.
Ukoo wa Jahazi hadi leo uko Uganda.
Mimi nilibahatika kukutana na Jahazi mmoja ambae alikuwa kiongozi wa wafanyakazi bandari ya Mombasa.
Katika mazungumzo aliniuliza kama namfahamu Dr. Jahazi.
Akaniambia kuwa ni ndugu yake.
Kulia ni Makanda Mwinyimkuu, Abushiri bin Salim na Jumbe Shomari Jahazi