Exaud J. Makyao
JF-Expert Member
- Nov 30, 2008
- 1,518
- 24
........................... ndiyo maana mtu haishii kutaja jina moja tu. Inabidi ataje majina zaidi ya moja ...................
Mimi nafikari ni sahihi kutaja majina na siyo kutaja jina. Kwa mfano ukiulizwa unaitwa nani na wewe ukajibu naitwa EXAUD, unakaribisha tena swali la pili kuwa, Exaud nani? Ili kukutofausha wewe na Exaud mwingine ndipo kunakopelekea kutaka majina mengine zaidi. Hata majina mawili bado yanaweza kutokukutambulisha sawa sawa hadi kuhitaji lingine la tatu au hata la nne.
Mkuu, usipige ikulu!KYACHAKICHE,
Mheshimiwa wazo lako linazua maswali pia.
Ukweli uko wapi sasa?
Kama ukiulizwa jina lako ni nani, unapaswa kutaja jina na siyo majina.
Kama ukisema jina lako ni KITAKACHO KUJA KIJE,
Mimi sioni kuwa umejibu ulichoulizwa kwa mujibu wa lugha ya kiswahili.
Jina ni umoja siyo wingi.
BABUYAO,
Hapa naona unanipa wakati mgumu zaidi.
Kwa nini mtu ataje majina zaidi ya moja wakati mtu mmoja anapaswa kuwa na jina moja?
Ukiulizwa jina lako nani , ukataja majina zaidi ya moja, kwangu inamaanisha umetaja na majina ya watu wengine.
Kwa kawaida, Jina la mtu, ni moja tu. Au?
Utifautishe mambo mawili: kuna suala la lugha, na pili kuna suala la ujumbe wenyewe.
Lugha: Kuulizwa jina moja ni namna ya kuongea kifasihi Kiswahili. Lakini ,,,,,,,,,,,,,,,,, Mswahili atakuuliza jina lako nani? akimaanisha siyo jina moja tu, bali na la pili , na la tatu, nk ili uweze kuji-identify bila ambiguity. Uwe bayana.
Mimi sijui wewe mwenzangu ni wa wapi lakini lugha nyingi za Kibantu zinatumia wingi kwa kumaanisha umoja. Je, hayo ni makosa kifasihi? Hapana! Mfano katika lugha nyingi unaweza kusikia (tafsiri tu) mtu anakuambia kwa kilugha "karibuni, jongeeni" wakati wewe ni mtu mmoja. Kwa nini wingi wakati mtu ni mmoja. Pia hata katika lugha za Kizungu, mf. Kijerumani na Kiitalia kuna namna hiyo ya kuongea. Hizi zinaitwa mode of expression. Zinakataa mantiki ya kawaida ya ku-reason kwa mstari ulionyooka. Ilikufahamu maana yake lazima uingie katika utamaduni wa watu, ujifunze namna yao ya kuongea.BABUYAO,
Turudi upande wa Lugha.
Unapotetea uhalali wa kutoa jibu la wingi katika umoja, lugha haikupi usahihi.
Hata wajukuu zako watachanganyikiwa.
Napata wazo kuwa, kutokana na mawazo yako, Lugha haina swali sahihi la kupata full identity ya mtu.
AU?
Mkuu kwa hapo tuko pamoja.Jina ni moja, lakini linaweza kuwa na maneno zaidi ya moja. Jina ni kitambulisho. Mtu mmoja anakuwa na jina moja. Augustine Moshi ni jina langu, na sio majina yangu.
Kwa wale Wakristo, nisemehe hivi: Yesu aliwaamuru wafuasi wake waende duniani kote wakiwabatiza watu kwa JINA la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Sio kwa MAJINA ya ......, kwani Mungu ni mmoja na jina lake ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni jina moja tu.
Kwa hivyo basi, anayechanganikiwa hapa ni yule anayedhani jina lazima liwe neno moja.
Jina ni moja, lakini linaweza kuwa na maneno zaidi ya moja. Jina ni kitambulisho. Mtu mmoja anakuwa na jina moja. Augustine Moshi ni jina langu, na sio majina yangu.
Kwa wale Wakristo, nisemehe hivi: Yesu aliwaamuru wafuasi wake waende duniani kote wakiwabatiza watu kwa JINA la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Sio kwa MAJINA ya ......, kwani Mungu ni mmoja na jina lake ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni jina moja tu.
Kwa hivyo basi, anayechanganikiwa hapa ni yule anayedhani jina lazima liwe neno moja.
AUGUSTINE, NA KYACHAKICHE,
Hapo siko pamoja nanyi.
Kusema kuwa Augustine Moshi ni jina lako, ni kama unalazimisha wewe binafsi kumiliki jina la ukoo wako.
Wewe ni Augustine, na Moshi ni jina la ukoo wako.
Wakuu tazameni ukweli huo.
Nadhani hajalazimisha hilo ndio jina lake, labda swali lilitakiwa kuuliza JINA LAKO KAMILI na si jina lako. Mtu hatambuliwa kwa jina moja, inatakiwa majina yake kamili.
Kaka Exaud, kwa jinsi ninavyo elewa mimi, haya mambo ya jina na mtu akakutajia majina mawili mpaka matatu, ni matokeo ya mazoea ya kitamaduni tulio rithi toka kwenye tanaduni zetu. Na vile vile inategemea na mazingira uliokuwepo wakati unaulizwa swali.KIJUNJWE,
Asante kwa mchango wako.
Hapa umeleta changamoto mpya,"JINA LAKO KAMILI" na "MAJINA YAKO KAMILI".
Utata huo ndo ulionipelekea kuona kuwa kuna haja ya kufikiri kama ni sahihi kumuuliza mtu jina lake halafu jibu lake liwe mlolongo wa majina.
Sasa naona umezidi kuchochea utata huu.
Waungwana,
Mtu jina lake ndilo linalomtambulisha yeye mmoja pekee katika kundi. Mathalan, mtu akisema jina lake John au Kidawa au Ali anakuwa hajajitambulisha kikakamilifu kwa kuwa ametumia jina la kawaida. Kuna akina John au Kidawa au Ali kibao. Na akitumia jina la ukoo pekee, kwa mfano Mazengo au Ng'wanakilala au Magohagasenga, hao nao wako kibao katika ukoo. Lakini mtu akijitambulisha kama John Robert Mazengo, hilo kiutambulisho linakuwa jina la mtu mmoja lililokamili na kiutaratibu linahesabiwa jina moja na kiihesabu yanakuwa majina matatu yanayomtambulisha mtu mmoja.
Kupanga ni kuchagua!
Napatwa utata pale mtu anapoulizwa jina lake au kuagizwa aandike jina lake, kisha anajibu au kuandika, mimi ni fulani fulani fulani ( John Alfa Mohamedi).
Ni sahihi mtu kujibu au kuandika majina matatu wakati kaulizwa JINA lake?