Hata kwa Kiingereza wanasema what is your name?. Hawasemi what are your names? Na jibu ni "my name is Augustine Moshi", na sio "my names are Augustine Moshi". Lugha za kikabila vile vile zinatambua Augustine Moshi kama jina langu, na sio majina yangu.
Nirudi tena kwenye Maandiko: Mungu alimwambia Musa kwamba jina lake ni I AM. Hilo ni jina la Mungu, na sio majina ya Mungu.
Ukipenda kuepukana na maswali mengi nenda Kenya. .....................QUOTE]
KIPALA,
Sidhani kama Kenya ni mfano mzuri wa mahali KISWAHILI kinatumiwa vizuri. Bado kiswahili ni kichanga sana huko Kenya.
Bado sijapata muafaka wa mada hii kuhusu JINA LAKO au MAJINA YAKO.