LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 18,037
- 33,681
Barani Afrika unaweza kujua kabila la mtu fulani kwa kuzingatia jina lake la ukoo. Mfano; Massawe ( Mchaga ), Mulokozi ( Muhaya ), Pazi ( Mzaramo ), Masanja ( Msukuma ), Mwaikimba ( Mnyakyusa ), Mwita ( Mkurya ), Onyango ( Mjaluo ), Mhina ( Msambaa ) , Ngonyani ( Mngoni ) na Mollel ( Mmasai ) kwa kutaja machache. Lakini uchunguzi wangu binafsi umeniwezesha kugundua kwa llipo jina moja la ukoo ambalo hutumiwa na zaidi ya makabila matano ya Afrika Mashariki , kusini na kati . Jina hilo ni " MBOGO ". Jina hili hutumiwa na :1. WANYAMWEZI .WASUKUMA wa MWASHITA ( Mwanza, Shinyanga Tabora ), 2. WANYATURU wa SINGIDA, 3. WANGONI wa RUVUMA 4. WAKURYA wa MARA. 5. Wazaramo wa Pwani 6. Wabondei wa Muheza na WAKIKUYU wa Nairobi Kenya... Hayo ni makabila ninayo yafahamu, inawezekana yapo makabila mengine yanayo tumia jina hili.. Jina hili lina maanisha kitu gani cha maana sana hadi kutumiwa na watu kutoka makabila mengi kiasi hiki?. Tujuzane waungwana.
" Ukisikia ndugu yako yuko polisi Chang'ombe, fanya mpango umtoe kabla hajafika ngome "
" Ukisikia ndugu yako yuko polisi Chang'ombe, fanya mpango umtoe kabla hajafika ngome "