Jina Palestina sio jina la kiarabu limetoka wapi ungana nami ujue limetoka wapi ni ndefu kidogo ila jitahidi kuisoma
ππππ
Miaka 300 kabla hajazaliwa Yesu kiliibuka kizazi chenye akili sana cha ugiriki hiki ndo kipindi socrates, aristostle, plato na alexander the great waliishi- hiki kilikuwa ni kipindi cha greek golden generation- greek ilikuwa inatawala duniani
Eneo la samaria na judea baada ya kuvunjwa kwa hekalu lilikuwa chini ya kina nebukadneza lilikuwa linatawaliwa kama koloni kutoka kwenye dola ya kina nebukadneza na kumbuka nebukadneza lilikuwa jina la watawala kama ilivyokuwa kwa pharao na herode
Kukua kwa greek walitaka kuongeza mipaka walikuwa na nguvu sana sasa moja ya dollar iliuyopitia wakati mgumu sana ni hii ya kina nebukadneza ilishambuliwa sana na greek na hata alexander the great alifika mpaka afganstan kwa sababu alikuwa anapigana vita na hatimaye greek walishinda
Sasa moja ya maeneo ambayo yalianguka ni eneo la samaria na judea kwa hiyo wagiriki walitaka kutawala kwa kuhakikisha watu wa eneo lile wana-adopt greek culture
Ila wayahudi waligomea haya mabadililo kupitia MACCABES REVOLT kupitia kiongozi mdogo aliyeitwa judas maccabes kitabu cha maccabes kipo kwenye biblia ya waroma na walishinda kwa hiyo wagiriki waliwaacha waendelee kufuata tamaduni zao ila still mtawala wa eneo alikuwa ni mgiriki
Wagiriki hawakukubali kushindwa kwa hiyo walifanya fitna kwa kumsupport mtu anayeitwa herode the great dhidi ya maccabes ambao walikuwa watawala wa wakati huo mwisho wa siku herode akashinda na ndo akawa mtawala
Herode katawala Yesu anazaliwa anauwa watoto wote wa kiume familia ya yesu inakimbilia misri anakufa anakuja mtoto wake herode wa pili anatawala kwa ubabe anafanyiwa fitna anaondolewa kuanzia hapa dola warumi kupitia wagiriki wanamteua PONTIO PILATO KAMA matwala wa eneo la judea na samaria ila utawala wa herode uliendelea ila kwa udogo sana hasa maeneo ya galilaya na nazareth ndo maana Yesu alipokuwa anasulubiwa alipelekwa kwa herode wa tatu ambaye ni mtwawala wa galilaya na nazareth
Hali ilendelea hivyo mpaka miaka ya 130' wayahudi waliraise against roma empire na walishinda kwa mda kupitia Simon bar Kokhba ambaye alikuwa ni masihi ila baada ya miaka 3 mbeleni dolla ya kirumi ilirudi na kumshinda simon bar kokhba na kubadilisha jina kutoka samaria na judea na kuwa palestina
Tokea mwaka wa 135 eneo hilo liliitwa palestina mpala leo hii na ni jina la kigiriki na sio kiarabu
Umeandika historia ndefu, lakini kuna jambo muhimu umelikosea:
jina Palestina halikuanza mwaka 135 BK.
Jina linalohusiana na
Palestine/Palaestina lilikuwa tayari linatumika kabla ya Hadrian. Baada ya uasi wa Bar Kokhba (132β136 BK), Warumi chini ya Kaisari Hadrian waliita jimbo la Yudea
Syria Palaestina, lakini hiyo haimaanishi kwamba Hadrian ndiye aliyeanzisha neno βPalestinaβ kwa mara ya kwanza.
Pia, kusema βPalestina ni jina la Kigiriki na si la Kiarabuβ hakuthibitishi kwamba ni jina lililotengenezwa na Wagiriki. Jina hilo lina uhusiano wa kale na
Philistia/Philistines, na aina mbalimbali za jina hilo zilitumika kabla ya Uislamu na kabla ya Warumi kulibadilisha Yudea kuwa Syria Palaestina.
Na kuna kosa jingine:
Bar Kokhba hakuwa βmasihiβ kwa maana kwamba historia imethibitisha alikuwa Masihi. Baadhi ya Wayahudi, akiwemo Rabbi Akiva kulingana na vyanzo vya kihistoria, walimwona kama Masihi, lakini huo ulikuwa mtazamo wa wafuasi wake.
Kwa hiyo usichanganye mambo mawili:
Warumi waliipa jimbo jina rasmi βSyria Palaestinaβ baada ya uasi wa Bar Kokhba β lakini neno Palestina lenyewe lilikuwa na matumizi ya zamani zaidi.
Kama unataka kubishana kihistoria, lete chanzo cha kale kinachosema kwamba
Hadrian ndiye aliyeuNDA jina βPalestinaβ mwaka 135 BK. Hapo ndipo hoja yako inaweza kupimwa.