Mwamgunda
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 247
- 48
Poleni na majukumu wapendwa! Wiki iliyopita niliandka thread hapa kuomba ushauri juu ya tatizo la kusumbuliwa na jino. Nilipewa ushauri na Mzizi Mkavu juu ya kukinga mkojo wangu na kusukutua kila niamkapo asubuhi kabla cjapiga mswaki na kukaa dk 10 ndo nipge mswaki, kimsingi nilipiga moyo konde na kufuata ushauri huo japo kiukweli yataka uwe na roho ngumu. Lakini mpaka sasa bado maumivu yapo palepale wapendwa, kiukweli nateseka na kung'oa nahisi ntakuwa kibogoyo ktk umri mdg kwani hapa nilipo nina miaka 25 nishang'oa meno 7. Je, kuna njia nyingne mbadala? Msaada tafadhalini ndg zangu, na mungu awabariki na kuwaongoza ktk kila jambo!