Jino la juu acha kabisa.

Hussein omari

Member
Joined
Aug 4, 2017
Posts
8
Reaction score
2
Habari wakubwa.? Jino lanisumbua Sana nakosa raha kabisa! Please tupeane msaada na maelezo pia mana nimetoa juzi na Leo mawili yanasumbua tena nini tiba ya hili?
 
Kwanza kabla sijatoa tiba, dawa ya jino sio kung'oa ila dawa yake nikulitibu. Mara nyingi ugonjwa wa meno husababishwa na bakteria wanaoathiri kinywa ndio mtu akashauriwa apige mswaki kila baada ya kula ama hususan usiku kabla ya kulala. Kwa tiba chukua mdaa, shabu na karafuu zote zikiwa unga na ujazo dawa changanya na utie kwa pamba na uweke sehemu ilioathirika. Utafanya Mara tatu kwa siku.
 
Mdaa na shabu ndo vitu gani?
 
Sasa hivi kila dawa nzuri ni ya Kiarabu tuu..
 
Mkuu meno yako yana bacterial infection ambao wanashambulia meno yako continously.. Muone dentist mapema atakupa dawa flani ivi ya maji ambayo itazuia hao bacteria kuendelea kushambulia meno yako.. hiyo dawa ni ya kusukutua ( Jina limenitoka kidogo)..
Usipofanya ivo haraka utang'oa yote ayo..

Nb: Meno yako yapo susceptible sana na kushambuliwa na bacteria... fanya hivi

1. Asubuhi
Piga mswaki vizuri na dawa kuzunguka meno yote..usisahau ulimi.

2.Mchana pia baada ya kula hakikisha unapiga tena au unasukutua vizuri kwa maji kinywa chako uondoe mabaki ya chakula though mswaki is highly recommended for best results.

3. Usiku
Kabla ya kulala piga tena mswaki meno na ulimi..

4. Punguza matumizi ya vyakula vyenye sukari nyngi kama pipi, biscut etc.. kwasababu hua vinacreate favourable condition for bacteria growth..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…