Jinsi 4R za Rais Samia zinavyoweza kutatua mgogoro wa DRC

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Ninapotafakari kwa kina mgogoro unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ninakumbuka falsafa ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan. Kama ingetekelezwa ipasavyo, inaonekana kuwa ingeweza kuumaliza mgogoro huu mara moja.

Swali linalojitokeza: Kwa nini wasaidizi wa Rais Samia hawachukui hatua kuhakikisha falsafa hii inatumika katika kutatua mgogoro huu?

Kazi ya kiongozi ni kuonyesha njia, kisha wengine wafuate. Rais Samia alipoingia madarakani, alikuta nchi ikiwa na changamoto za kisiasa, na akaja na falsafa yake ya 4R kama suluhisho la kuzitatua. Mgogoro wa DRC unaohusisha waasi wa M23 pia ungeweza kushughulikiwa kupitia falsafa hii na kufikia suluhisho la haraka.

Falsafa ya 4R inajikita katika misingi ya: Maridhiano (Reconciliation), Ustahimilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms) na Ujenzi wa Taifa upya (Rebuilding).

Kinachoendelea DRC ni matokeo ya mgogoro wa muda mrefu. Serikali ya DRC inahesabu M23 kama waasi wa Kinyarwanda na inataka waondoke kwenye ardhi yake. Kwa upande mwingine, M23 wanajitambua kama Wanyamulenge, wakazi wa asili wa Goma, hivyo hawaoni sababu ya kuondoka. Rwanda inaunga mkono madai yao ili wapate haki yao ya kutambuliwa.

Fursa kwa Tanzania katika usuluhishi

Wiki iliyopita, nilimpongeza Rais Samia kwa kuitisha mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na EAC kujadili mgogoro wa DRC. Hata hivyo, nilisikitika kuona kuwa taarifa za mkutano huo zilitolewa kwa Kiingereza, Kifaransa na Kireno pekee, bila Kiswahili. Tanzania, ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo, inatumia Kiswahili, Goma ni eneo linalotumia Kiswahili, na hata waasi wa M23 wanazungumza Kiswahili. Kwa nini basi Kiswahili kimepuuzwa?

Pia, mkutano huo ulijadili mgogoro wa DRC bila kuwahusisha waasi wa M23, jambo ambalo ni makosa. Haiwezekani kupata suluhisho la mgogoro bila kuwashirikisha wahusika wakuu. Hatua ya kwanza katika usuluhishi ni maridhiano na kusitisha vita.

Mgogoro huu ni fursa adhimu kwa Tanzania kuonyesha uwezo wake wa kutatua matatizo ya Afrika kwa njia za Kiafrika. Ikiwa 4R zitatumika kwa ufanisi, Rais Samia ataonyesha kuwa Tanzania inaweza kuwa kinara wa suluhisho za Kiafrika kwa migogoro ya bara hili.

Njia ya kutatua mgogoro wa DRC kwa 4R ni pamoja na maridhiano (Reconciliation) – Serikali ya DRC inapaswa kukubali kuwa M23 ni sehemu ya raia wake na kufanya mazungumzo ya maridhiano ili kusitisha vita. Lakini pia ustahimilivu (Resilience), yaani DRC inapaswa kujifunza kuvumilia na kukubali uwepo wa raia wake wenye asili ya Rwanda. Vilevile, M23 wanapaswa kuonyesha ustahimilivu kwa kusitisha mapambano na kukubali mazungumzo. Njia nyingine nia mageuzi (Reforms), yaani M23 waachane na jina la waasi na badala yake waonekane kama jeshi la ukombozi wa Banyamulenge. Lazima kufanyike mageuzi ya kijeshi na kisha M23 waingizwe rasmi ndani ya jeshi la DRC.

Na mwisho ni ujenzi wa Taifa upya (Rebuilding), DRC inapaswa kujengwa upya kama taifa lenye mshikamano, linalowahusisha raia wake wote bila ubaguzi wa asili.

Ikiwa falsafa ya 4R itatumika ipasavyo, mgogoro huu unaweza kutatuliwa ndani ya muda mfupi. Suluhisho la kweli linatokana na ukweli kwamba M23 ni sehemu ya DRC na wanapaswa kushirikishwa katika ujenzi wa amani badala ya kuendelea na vita. Rwanda na Uganda zitaacha kuwaunga mkono M23 pindi DRC itakapokubali ukweli huu na kufanya maridhiano ya kweli.

Rais Samia ana nafasi ya pekee ya kulitatua hili kwa kutumia falsafa yake. Ikiwa hatua sahihi zitachukuliwa, Tanzania itang'ara kimataifa kama taifa linaloweza kutoa suluhisho kwa migogoro ya Afrika.

Nimemtwisha Rais Samia jukumu la kuutatua mgogoro huu, kwasababu mgogoro huu ni fursa adhimu kwa Tanzania na Rais Samia,Kiafrika,kikanda na kimataifa,kuiambia dunia matatizo ya Afrika,yanahitaji
suluhisho la ki Afrika na Afrika,tuna viongozi wenye uwezo wa kuutatua mgogoro kia Afrika。

Pia kumalizika kwa mgogoro huu ni fursa ya kiuchumi kwa Tanzania kupitia Dar Port

Hili Mama analiweza na liko ndani ya uwezo wake!。

Hili mnalionaje?

Mungu mbariki Rais Samia, Mungu ibariki Tanzania.

Chanzo: Mwananchi
 
Attachments

  • Congo .png
    Congo .png
    491.6 KB · Views: 2
focus na nguvu yao imeelekezwa oktoba 2025 sidhani kama watakuwa na muda wa kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya drc.
 
Kutatua migogoro ya Nchi za maziwa makuu, inahitaji tahadhari ya Hali ya juu. Kikwete alijaribu kwa Rwanda yakamkuta.

Mwalimu Nyerere Naye alijaribu Burundi, mwishowe akamuachia Mkapa!
 
Wanabodi,

https://www.mwananchi.co.tz/mw/haba...weza-kuwa-suluhisho-la-mgogoro-wa-drc-4932360 Nimemtwisha Rais Samia jukumu la kuutatua mgogoro huu, kwasababu mgogoro huu ni fursa adhimu kwa Tanzania na Rais Samia,Kiafrika,kikanda na kimataifa,kuiambia dunia matatizo ya Afrika,yanahitaji
suluhisho la ki Afrika na Afrika,tuna viongozi wenye uwezo wa kuutatua mgogoro kia Afrika。

Pia kumalizika kwa mgogoro huu ni fursa ya kiuchumi kwa Tanzania kupitia Dar Port

Hili Mama analiweza na liko ndani ya uwezo wake!。

Hili mnalionaje?

Paskali
Hapa Advocate unapuyanga.
Huu mgogoro VS 4R????
Kagame amekaza sana nati na kasema yupo teyari kwa vita anytime.
 
Wanabodi,

https://www.mwananchi.co.tz/mw/haba...weza-kuwa-suluhisho-la-mgogoro-wa-drc-4932360 Nimemtwisha Rais Samia jukumu la kuutatua mgogoro huu, kwasababu mgogoro huu ni fursa adhimu kwa Tanzania na Rais Samia,Kiafrika,kikanda na kimataifa,kuiambia dunia matatizo ya Afrika,yanahitaji
suluhisho la ki Afrika na Afrika,tuna viongozi wenye uwezo wa kuutatua mgogoro kia Afrika。

Pia kumalizika kwa mgogoro huu ni fursa ya kiuchumi kwa Tanzania kupitia Dar Port

Hili Mama analiweza na liko ndani ya uwezo wake!。

Hili mnalionaje?

Paskali
Looh! Bw. Paskali naona unaota Sasa.
Mgogoro wa DRC (Zaire) ni mfupa mgumu. Mgogoro huo una historia ndefu Sana ya tangu miaka mingi kuanzia huko mwanzoni mwa miaka ya 1960s.

Bad enough if not a worse enough, kwa Sasa hakuna Mtawala yoyote yule wa kutoka katika nchi za Afrika ambaye ni msafi na ambaye mwenye uwezo wa kutatua huo Mgogoro wa huko DRC. Watawala karibia wote kabisa waliopo barani Afrika kwa Sasa hawana moral authority ya kuweza kumkemea Paul Kagame au Waasi wa M23 ili waache kuipiga Vita Utawala wa DRC (Zaire) kwa sababu kila mmoja nchini mwake ana makandokando yake Kama hayo hayo yaliyopo huko Zaire au ana matatizo mengine yanayofanana kwa karibu na Yale matatizo yaliyopo huko Zaire ambayo yamewalazimisha Waasi wa M23 kutaka kuupindua Utawala wa huko.
Mwl. Nyerere na Nelson Mandela walikuwa na uwezo wa kutatua migogoro ya namna hiyo kwa sababu wao wenyewe kwa kiasi kikubwa walikuwa wasafi na walikuwa wanaheshimika na kuaminika na Watu wengine.

Doctrine of Equity states that "He who goes for equity must go with clean hands."
 
Fursa ilikuwepo lakini imetiwa dosari na sisi kutuma jeshi letu kuungana na majeshi ya SADC kwa lengo la kwenda kupigana na makundi yaliyoasi huko DRC hasa M23.
Ulikuwa uamuzi usiokuwa wa busara kwa nchi mwanachama wa EAC kwenda vitani kuishambulia nchi nyingine ambayo pia ni mwanachama wa EAC kwa mwavuli wa SADC.
Hii ni blunder kubwa kidiplomasia ambayo haikupaswa kufanyika hadi kugharimu maisha ya wanajeshi wetu.

Hizo R4 zibakie tu humu humu ndani ya mipaka yetu kama fimbo na karoti ya kuendesha siasa za ushindani dhidi ya wapinzani.
 
Kwamba ni kama kidonge watu wakimeza wanapona ?!!!

Ideas is one thing..., Implementation is the King...

Na haya mambo yanadilute Hoja hivi 4R za Samia ndio nini ? Yaani ni kama Archimedes Principle yeye ndio brain child yake au ni mambo ya kawaida kabisa ambayo yanajulikana tangia zama za mawe ?
 
Kaka pasco bwana yani ya kwako nyumbani yamekushinda unataka ya jirani kuyaweza.

Ushaona wapi aliyekosa akili hakawa mfano
 
Huyo maza ameshindwa kutatatua mambo ya ndani kwake kama katiba na tume huru,utekakaji na kupotezana ndo hataweza ya vita vya jirani?
Yupo soft mno!
 
Hii ndio unaona kbs kwamba hata waliopata elimu bado wanapata tabu ktk kuchanganua mambo na kuyaelewa, mama katoa wapi uwezo na utashi wa kudeal na mambo magumu kiasi hicho?
 
Wanabodi,

Ninapotafakari kwa kina mgogoro unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ninakumbuka falsafa ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan. Kama ingetekelezwa ipasavyo, inaonekana kuwa ingeweza kuumaliza mgogoro huu mara moja.

Swali linalojitokeza: Kwa nini wasaidizi wa Rais Samia hawachukui hatua kuhakikisha falsafa hii inatumika katika kutatua mgogoro huu?

Kazi ya kiongozi ni kuonyesha njia, kisha wengine wafuate. Rais Samia alipoingia madarakani, alikuta nchi ikiwa na changamoto za kisiasa, na akaja na falsafa yake ya 4R kama suluhisho la kuzitatua. Mgogoro wa DRC unaohusisha waasi wa M23 pia ungeweza kushughulikiwa kupitia falsafa hii na kufikia suluhisho la haraka.

Falsafa ya 4R inajikita katika misingi ya: Maridhiano (Reconciliation), Ustahimilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms) na Ujenzi wa Taifa upya (Rebuilding).

Kinachoendelea DRC ni matokeo ya mgogoro wa muda mrefu. Serikali ya DRC inahesabu M23 kama waasi wa Kinyarwanda na inataka waondoke kwenye ardhi yake. Kwa upande mwingine, M23 wanajitambua kama Wanyamulenge, wakazi wa asili wa Goma, hivyo hawaoni sababu ya kuondoka. Rwanda inaunga mkono madai yao ili wapate haki yao ya kutambuliwa.

Fursa kwa Tanzania katika usuluhishi

Wiki iliyopita, nilimpongeza Rais Samia kwa kuitisha mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na EAC kujadili mgogoro wa DRC. Hata hivyo, nilisikitika kuona kuwa taarifa za mkutano huo zilitolewa kwa Kiingereza, Kifaransa na Kireno pekee, bila Kiswahili. Tanzania, ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo, inatumia Kiswahili, Goma ni eneo linalotumia Kiswahili, na hata waasi wa M23 wanazungumza Kiswahili. Kwa nini basi Kiswahili kimepuuzwa?

Pia, mkutano huo ulijadili mgogoro wa DRC bila kuwahusisha waasi wa M23, jambo ambalo ni makosa. Haiwezekani kupata suluhisho la mgogoro bila kuwashirikisha wahusika wakuu. Hatua ya kwanza katika usuluhishi ni maridhiano na kusitisha vita.

Mgogoro huu ni fursa adhimu kwa Tanzania kuonyesha uwezo wake wa kutatua matatizo ya Afrika kwa njia za Kiafrika. Ikiwa 4R zitatumika kwa ufanisi, Rais Samia ataonyesha kuwa Tanzania inaweza kuwa kinara wa suluhisho za Kiafrika kwa migogoro ya bara hili.

Njia ya kutatua mgogoro wa DRC kwa 4R ni pamoja na maridhiano (Reconciliation) – Serikali ya DRC inapaswa kukubali kuwa M23 ni sehemu ya raia wake na kufanya mazungumzo ya maridhiano ili kusitisha vita. Lakini pia ustahimilivu (Resilience), yaani DRC inapaswa kujifunza kuvumilia na kukubali uwepo wa raia wake wenye asili ya Rwanda. Vilevile, M23 wanapaswa kuonyesha ustahimilivu kwa kusitisha mapambano na kukubali mazungumzo. Njia nyingine nia mageuzi (Reforms), yaani M23 waachane na jina la waasi na badala yake waonekane kama jeshi la ukombozi wa Banyamulenge. Lazima kufanyike mageuzi ya kijeshi na kisha M23 waingizwe rasmi ndani ya jeshi la DRC.

Na mwisho ni ujenzi wa Taifa upya (Rebuilding), DRC inapaswa kujengwa upya kama taifa lenye mshikamano, linalowahusisha raia wake wote bila ubaguzi wa asili.

Ikiwa falsafa ya 4R itatumika ipasavyo, mgogoro huu unaweza kutatuliwa ndani ya muda mfupi. Suluhisho la kweli linatokana na ukweli kwamba M23 ni sehemu ya DRC na wanapaswa kushirikishwa katika ujenzi wa amani badala ya kuendelea na vita. Rwanda na Uganda zitaacha kuwaunga mkono M23 pindi DRC itakapokubali ukweli huu na kufanya maridhiano ya kweli.

Rais Samia ana nafasi ya pekee ya kulitatua hili kwa kutumia falsafa yake. Ikiwa hatua sahihi zitachukuliwa, Tanzania itang'ara kimataifa kama taifa linaloweza kutoa suluhisho kwa migogoro ya Afrika.

Nimemtwisha Rais Samia jukumu la kuutatua mgogoro huu, kwasababu mgogoro huu ni fursa adhimu kwa Tanzania na Rais Samia,Kiafrika,kikanda na kimataifa,kuiambia dunia matatizo ya Afrika,yanahitaji
suluhisho la ki Afrika na Afrika,tuna viongozi wenye uwezo wa kuutatua mgogoro kia Afrika。

Pia kumalizika kwa mgogoro huu ni fursa ya kiuchumi kwa Tanzania kupitia Dar Port

Hili Mama analiweza na liko ndani ya uwezo wake!。

Hili mnalionaje?

Mungu mbariki Rais Samia, Mungu ibariki Tanzania.

Chanzo: Mwananchi
Labda zitatue mfuko wa hazina ya fedha za umma. Hapo zinatatua kweli kweli.
 
Vipi kuhusu external factors? M23 hawajafika tu pale wenyewe. Kwa mfano kwa sasa kuna ushahidi kwamba askari na maafisa wa jeshi la Rwanda wanapigana na majeshi ya DRC wakiwa kwenye kivuli cha M23.

Na sababu ya Rwanda pamoja na wageni wengine kufanya hivyo ni kulinda maslahi yao ya kiuchumi wanayoyapata kutokana na kuvurugika kwa amani eneo la mashariki ya DRC.

M23 na wachimbaji wote wa madini haramu huko mashariki ya DRC wanayauza Kigali.

Sasa hizo external factors zinamalizwa vipi na 4R za Mheshiwa mwenyekiti wetu?

Wakati fulani vita ndio suluhu ya tatizo. Ndio maana hata Mungu wetu ni BWANA wa majeshi na Mungu wa vita. Alitumia vita mara nyingi tu kuwafikisha watu wake anapopataka.

DRC wawekeze kwenye jeshi lao kisha wapigane vita ya kukata maneno. Vita moja ya mwisho itakayommaliza adui moja kwa moja.
 
Wanabodi,

Ninapotafakari kwa kina mgogoro unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ninakumbuka falsafa ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan. Kama ingetekelezwa ipasavyo, inaonekana kuwa ingeweza kuumaliza mgogoro huu mara moja.

Swali linalojitokeza: Kwa nini wasaidizi wa Rais Samia hawachukui hatua kuhakikisha falsafa hii inatumika katika kutatua mgogoro huu?

Kazi ya kiongozi ni kuonyesha njia, kisha wengine wafuate. Rais Samia alipoingia madarakani, alikuta nchi ikiwa na changamoto za kisiasa, na akaja na falsafa yake ya 4R kama suluhisho la kuzitatua. Mgogoro wa DRC unaohusisha waasi wa M23 pia ungeweza kushughulikiwa kupitia falsafa hii na kufikia suluhisho la haraka.

Falsafa ya 4R inajikita katika misingi ya: Maridhiano (Reconciliation), Ustahimilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms) na Ujenzi wa Taifa upya (Rebuilding).

Kinachoendelea DRC ni matokeo ya mgogoro wa muda mrefu. Serikali ya DRC inahesabu M23 kama waasi wa Kinyarwanda na inataka waondoke kwenye ardhi yake. Kwa upande mwingine, M23 wanajitambua kama Wanyamulenge, wakazi wa asili wa Goma, hivyo hawaoni sababu ya kuondoka. Rwanda inaunga mkono madai yao ili wapate haki yao ya kutambuliwa.

Fursa kwa Tanzania katika usuluhishi

Wiki iliyopita, nilimpongeza Rais Samia kwa kuitisha mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na EAC kujadili mgogoro wa DRC. Hata hivyo, nilisikitika kuona kuwa taarifa za mkutano huo zilitolewa kwa Kiingereza, Kifaransa na Kireno pekee, bila Kiswahili. Tanzania, ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo, inatumia Kiswahili, Goma ni eneo linalotumia Kiswahili, na hata waasi wa M23 wanazungumza Kiswahili. Kwa nini basi Kiswahili kimepuuzwa?

Pia, mkutano huo ulijadili mgogoro wa DRC bila kuwahusisha waasi wa M23, jambo ambalo ni makosa. Haiwezekani kupata suluhisho la mgogoro bila kuwashirikisha wahusika wakuu. Hatua ya kwanza katika usuluhishi ni maridhiano na kusitisha vita.

Mgogoro huu ni fursa adhimu kwa Tanzania kuonyesha uwezo wake wa kutatua matatizo ya Afrika kwa njia za Kiafrika. Ikiwa 4R zitatumika kwa ufanisi, Rais Samia ataonyesha kuwa Tanzania inaweza kuwa kinara wa suluhisho za Kiafrika kwa migogoro ya bara hili.

Njia ya kutatua mgogoro wa DRC kwa 4R ni pamoja na maridhiano (Reconciliation) – Serikali ya DRC inapaswa kukubali kuwa M23 ni sehemu ya raia wake na kufanya mazungumzo ya maridhiano ili kusitisha vita. Lakini pia ustahimilivu (Resilience), yaani DRC inapaswa kujifunza kuvumilia na kukubali uwepo wa raia wake wenye asili ya Rwanda. Vilevile, M23 wanapaswa kuonyesha ustahimilivu kwa kusitisha mapambano na kukubali mazungumzo. Njia nyingine nia mageuzi (Reforms), yaani M23 waachane na jina la waasi na badala yake waonekane kama jeshi la ukombozi wa Banyamulenge. Lazima kufanyike mageuzi ya kijeshi na kisha M23 waingizwe rasmi ndani ya jeshi la DRC.

Na mwisho ni ujenzi wa Taifa upya (Rebuilding), DRC inapaswa kujengwa upya kama taifa lenye mshikamano, linalowahusisha raia wake wote bila ubaguzi wa asili.

Ikiwa falsafa ya 4R itatumika ipasavyo, mgogoro huu unaweza kutatuliwa ndani ya muda mfupi. Suluhisho la kweli linatokana na ukweli kwamba M23 ni sehemu ya DRC na wanapaswa kushirikishwa katika ujenzi wa amani badala ya kuendelea na vita. Rwanda na Uganda zitaacha kuwaunga mkono M23 pindi DRC itakapokubali ukweli huu na kufanya maridhiano ya kweli.

Rais Samia ana nafasi ya pekee ya kulitatua hili kwa kutumia falsafa yake. Ikiwa hatua sahihi zitachukuliwa, Tanzania itang'ara kimataifa kama taifa linaloweza kutoa suluhisho kwa migogoro ya Afrika.

Nimemtwisha Rais Samia jukumu la kuutatua mgogoro huu, kwasababu mgogoro huu ni fursa adhimu kwa Tanzania na Rais Samia,Kiafrika,kikanda na kimataifa,kuiambia dunia matatizo ya Afrika,yanahitaji
suluhisho la ki Afrika na Afrika,tuna viongozi wenye uwezo wa kuutatua mgogoro kia Afrika。

Pia kumalizika kwa mgogoro huu ni fursa ya kiuchumi kwa Tanzania kupitia Dar Port

Hili Mama analiweza na liko ndani ya uwezo wake!。

Hili mnalionaje?

Mungu mbariki Rais Samia, Mungu ibariki Tanzania.

Chanzo: Mwananchi
Kuna makundi mengine zaidi ya M23 pale DRC kama FDLR na wahutu waliozaliwa DRC nayo yanahitaji suluhu.

Ili kumaliza huu mgogoro kabisa Kagame achukue ushauri wa Kikwete na kuanzisha maongezi ya amani na FDLR.
 
Back
Top Bottom