Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Mueleko wa nchi za Africa katika upande wa uchumi kuhusiana na madeni kwa miaka ya mbeleni sio mzuri sana.
Nchi takribani 20 za Africa zinakabiliwa na changamoto kubwa ya madeni, hii ni kutokana na ukopaji wa juu sana katika miaka 10 iliyopita. Hali tayari imepelekea nchi 3 (Ghana, Zambia na Ethiopia) kushindwa kulipa baadhi ya madeni yake kwa wakati hivi karibuni na kupelekea kukaa chini na wakopeshaji wake kufanya "debt restructuring"
Hali hii pia itawafanya wakopeshaji wengi kuongeza gharama za mikopo yao kwa maana ya riba kwa nchi nyingi nyingi za Afrika, hii ina maana nchi nyingi za Africa zitazidi kuongezekwa na mzigo wa madeni wa kulipa.
Tatizo lingine ni kwamba haya madeni yanayochukuliwa hayazalishi ajira za kutosha, hayaongezi sana kipato cha mtu mmoja mmoja au taifa kwa ujumla na matokeo yake ni kwamba sehemu kubwa mapato yanayopatikana yanaenda kulipa madeni huku pesa inayobaki kwa ajili ya kufanya maendeleo kuwa kidogo sana. Kenya tayari imeshaingia kwenye utando huu, kwenye bajeti ya sasa ya Kenya zaidi ya nusu ya bajeti ni kwa ajili ya kulipa madeni. Serikali imeona njia pekee ni kukamua raia kodi na raia nao wamechoka na wamekataa.
Kadri rushwa, matumizi ya anasa na yasiyo ya kipaumbele yatakavyoachiwa kutamalaki kwenye nchi nyingi za Africa hali itazidi kuwa mbaya sana kwa raia wa kawaida kwani njia ya kuifanya nchi iendeshwe ni kodi au mikopo tu, kila mmoja atafikiwa kwa wakati wake na matokeo ya hali hiyo.